Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuwataka watumishi wa wizara hiyo waliokuwa wakilitumia jengo la Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuhamisha ofisi zao na kuliacha kwa ajili ya matumizi ya wodi ya wazazi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hospitali hiyo, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka kufikia kesho tayari jengo hilo litakuwa limeanza kutumika kwa kuwa watafanya kazi ya kuhamisha makabrasha ya watumishi hao usiku kucha kuhakikisha agizo la Rais John Magufuli linatekelezwa mara moja.
bravo mh magufuli tunapenda kuona utendaji kama huo na bei ya vyakula tunataka ishuke
ReplyDeleteTunamshukuru mungu kwa kututeulia magufuli
ReplyDeleteMzigo waziri
ReplyDeleteKwani alipokwenda kumuona mufriti hakuchunguza haya
Magufuli hawa mawaziri wanaongozwa Na Na wasaidizi wao fukuza
Inaelekea awamu ina ufisadi kwenye vyombo vya habari ili waonekanekani wanafanya kazi
ReplyDeleteNyinyi vyombo habari nafikiri mna kitu hapa
Fichueni Na maovu Yao
Magufuli unaendesha nchi kwa media ?