Ubuyu! Tumbuatumbua ya majipu ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ inadaiwa kumtisha mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuja kuishi Bongo ikidaiwa kisa ni utajiri mkubwa alionao wenye shaka juu ya malipo ya ushuru na mapato.
Habari kutoka kwenye chanzo cha ndani cha familia ya Diamond, zimeeleza kuwa Zari alikuwa na mpango wa kuhamishia miradi na makazi yake rasmi Dar mwanzoni mwa mwaka 2016 lakini ndoto hiyo inaonekana kuyeyuka.
Chanzo hicho kilieleza kuwa, familia ya Diamond imekuwa ikimshinikiza jamaa huyo amshawishi Zari kuwekeza Bongo lakini kwa sasa mpango huo umefutika kwani mwanadada huyo anaogopa kutumbuliwa majipu.
“Unajua Zari anafuatilia kila kitu kinachoendelea nchini. Kwa hiyo usidhani hajui mambo ya TRA (Mamlaka ya Mapato) yalivyochachamaa.
“Unajua anasema akihamia Bongo itabidi aingize nchini yale magari yake ya kifahari anayotembelea akiwa Sauz (Afrika Kusini) au Uganda lakini anahofia tumbua majipu ya Magufuli.
“Wewe fikiria kama lile Range (Rover) la Wema (Sepetu) limekamatwa na TRA, itashindikana nini kukamata Hummer au Lamborghini ya Zari?
“Nafikiri ishu ni utajiri wake. Nilishasoma kwenye vyombo vya habari vya Uganda kuwa utajiri wake wa ghafla umekuwa ukiibua sana maswali na yeye huwa hapendi kuzungumzia vyanzo vya utajiri wake,” kilinyetisha chanzo chetu.
Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, mwanahabari wetu alithibitisha kuwa kweli Zari hayupo Bongo yupo Sauz hivyo alimsaka Diamond ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Zari ana miradi mingi, muda wa kuwekeza Bongo ukifika atakuja kufanya hivyo.
uhusu mheshimiwa (Magufuli) mimi nampongeza kwa kutumbua majipu kwa sababu tulikuwa tunahitaji kiongozi kama yeye,” alisema Diamond na kuongeza kuwa mpango wa Zari wa kuja kuishi Dar upo palepale.
Safi sn mrembo tunapenda w.wake kama nyinyi mbele mbele daima kuchapa kazi then spend
ReplyDeletefix. aishi bongo na mali za Ivan atazipataje.
ReplyDeleteUONGO HAWEZI KUJA ISHI BONGO. ANAJUA ANAKUMBANA NA WAKE WENZA WENGI. KAJALA UPOOOOOOOOOOOO.
ReplyDeletehe! safari kaja cku 2 tuu. bongo hapakaliki kiki kweshney.
ReplyDeletemali zenyewe za Ivan atazihamisha vipi. acheni uongo.
ReplyDeleteNapendaga udaku ukuna ufagio humu kumbe sio zake.Kama mzungu Na mkwewe
ReplyDeleteNa baby anahitaji viazi Na supu ya kuku ulyochanganywa Na mbogamboga apate mwili kidogo maana kadhoofu sn au nimezoea wangu wa kibongobongo uji wa ulezi asubuhi Na usiku ushauri wa bure
ReplyDeleteatutokee hapa nani anavitaka vitu vya Ivan. kashindwa kukaa ug. ataweza dar.
ReplyDeleteNA WATOTO 3 WOOTE WATAKUJA BONGO DAI ANAKAZI YA ZIADA
ReplyDeleteBibi, mjukuu, na kinyinginyi wanapeana mawazo jinsi ya kuficha DNA.
ReplyDeleteWabongo kwa umbea,waacheni na maisha yao
ReplyDeleteWabongo kwa umbea waacheni na maisha yao
ReplyDelete