Wakati baadhi ya vyama vya siasa vimetangaza kujitoa uchaguzi wa marudio Zanzibar, tume ya uchaguzi -ZEC- imetoa msimamao wake na kusema wagombea wote ni halali na watagombea nafasi zao kwa vile hakuna hata chama kimoja kilichofuata sheria na kanuni za uchaguzi.
Msimaamo huo wa tume umetolewa na mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salum Jecha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo amesema kuna utaratibu wakujitoa na kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi hakuna chama kilichofuata kanuni ikiwa ni pamoja na wadhamini wawagombea kutangaza kuondoa udhamini wao, hivyo wagombea wote wa urais, uwakilshi na udiwani wote bado ni halali.
Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi vyama amabvyo vimethibitisha kushiriki ni pamoja na CCM, TADEA, ADC, CCK, AFP, SAU, TLP, huku CUF, NRA, CHAUMA, DP, Jahazi asilia na ACT Wazalendo ambao mgombea wake Khamis Lilla ametangaza kugombea huku chama chake kikimufukuza uanachama.