Zitto Kabwe Ampa Laivu Rais 'Wanaokusifia tu Hawakusaidii'

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa watu wanaomsifia tu Rais Magufuli hawawezi kumsaidia katika kufikia malengo yake ya kuleta maendeleo na mabadiliko kwa taifa hili.

Zitto Kabwe aliweka wazi hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema anashukuru kuona Rais Magufuli anawasikiliza PIA watu ambao wanamkosoa kwa malengo mazuri kwani wana nia njema na wanatumia uzalendo wao wa hali ya juu kukosoa.

"Rais Wanaokusifia tu hawakusaidii. Umefanya vema kusikiliza tunaokukosoa. Tuna nia njema na tunatimiza uzalendo wa hali ya juu ambao ni kukosoa. Hatusemi wasikusifie, hapana. Wawe na kiasi" Aliandika Zitto Kabwe.

Siku za karibuni Zitto Kabwe aliandika Makala ya mambo kumi ambayo Rais Magufuli hajafanya ndani ya siku 100 na katika makala yake, jambo la nne alizungumzia suala la uingizwaji wa sukari kutoka nje na kusema ni jipu ambalo limeiva na linatakiwa kutumbuliwa.

"Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na serikali haina mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika mpango wa maendeleo serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa sukari ni jipu" Zitto Kabwe

Lakini Rais Magufuli ni kama amesikia kilio cha Mh Zitto Kabwe kwani tayari ametangaza kufutwa kwa vibali vya uingizwaji wa sukari nchini, jambo ambalo Mh Zitto amemshukuru Rais kwa kuliona na kulifanyia kazi na kumuomba pia aliangalie suala la IPTL/PAP nalo bila kulionea kigugumizi chochote.

"Rais Magufuli nakupongeza kwa kuona tusemayo wapinzani wa chama chako. Umetekeleza jambo 1/10 niliyoeleza kuwa hujafanya. Naomba utekeleze na hayo mengine kwa manufaa ya nchi yetu. Hili la IPTL/PAP mbona unalipatia kigugumizi ndugu Rais?
Umetoa agizo kuhusu hili. Shukrani sana" Aliandika Zitto Kabwe.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zitto kikoje cha kuumia akisifiwa raisi wetu wewe saizi yako Said Kubenea ya Magufuli hayakuhusu tumikia jimbo lako mbona hatujasikia watu wako wanakusifia wewe ni selfish inakusumbua na kutafuta kiki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu kijana anasumbuka na mengi. itabidhi tumchukulie hatu za nidhanmu lugha anayoitumia ina kasoro dhahiri na maeditor inabidi wapitie na kyridhuka na lugha ikiwemo ma tiki na maudhu ya mwandishi halafu vichwa vya habari wasicijyze ajili ya kycuria biashara

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad