Acheni Kumuonea Huruma Chidi Benz Anavuna Alichokipanda...Mnunuzi na Muuzaji Wote Waalifu-Faiza Ally

Katika ukurasa wake wa Instagram Faiza ameandika huku akiwapondea wale wanaomsikitikia, na kusema kuwa Chid amejichagulia mwenyewe kuwa hivyo kwani kabla hajaanza kutumia alikuwa anafahamu madhara yake.

“Kila mtu anamsikitikia Chidi kwa nini? Chidi sio mtoto ni maisha aliyo chagua, pengine unaweza kumsikitia mtoto aliye jifunza akiwa chini ya miaka 18 lakini sio mtu mzima! Kila siku mifano tunaiona jinsi gani madawa yana haribu watu inaama hawaoni ? Hawasikii ?"
Faiza ameendelea kuandika
 "Hapana kwa kweli mimi naona unavuna unachokipanda. Unapo sema ugumu wa maisha ndiyo umekupeleka kuvuta madawa au kuuza - hivi mnazani wote tunao cheka maisha yetu mepesi? Kwa kweli ni uzembe......! acheni kabisa kuwahurumia watu kijinga, lazima wajue wamekosea sio kuwa peti peti”.

Pamoja na hayo Faiza ameonekana kuchukizwa na kitendo cha biashara ya madawa ya kulevya inayoendelea nchini, na kutaka watumiaji na wauzaji pia wafungwe iwapo watathibitika, ili kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya.

“Hivi kwa nini wanao nunua madawa pia wasifungwe ??? Kwa sababu mtazamo wangu unaona mnunuzi na muuzaji wote ni wahalifu!

Kati ya hawa watu wawili wote wanafanya biashara maana kama hamna mnunuzi hakuna muuzaji, kama hakuna muuzaji hamna mnunuzi”, aliandika Faiza.

Pamoja na hayo Faiza amemtakia heri Chidi Benzi katika mapambano yake na kuachana na madawa ya kulevya, ili aweze kurudi kama zamani.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Usiongee hivyo faiza hujafa hujaumbika yeye ni binaadam kama binaadam mwengine hakuna aliyekamilika anything can happen na kama weweni muislsm kaisome vzuri qur-an M/mungu anasema hakika nafsi inaamrisha maovu isipokua kwa wale waliorehemewa kwa hiyo binaadam
    Anaweza akakosea taimu yoyote.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau hakuna cha uislam wala ukristo hapo,nafsi inaamrisha maovu na itakushinda kama utajiendekeza,kwa maana Mungu ametupa mamlaka ya kutambua baya na zuri.

      Delete
  2. Chidi amepiga about turn... Inakubalika. Wangapi ambao watoto wao watumia madawa ya kulevya watamani kama sasahivi wakubali kuwacha? Faiza bado uko hai labda umezaa labda uko na ndugu.. Hujafa hujaumbika

    ReplyDelete
  3. big up sana faiza, watu wakiwa na afya zao na vipesa kidogo huwa hawasikii la mtu..ni mara nyingi alikuwa akishauriwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya lakini hakusikia, alisema tuache kumfuatafuata na maisha yake...sasa baada ya kuharibikiwa ndiyo anarudi kuomba msaada kwetu... acha akome amevuna alichopanda...

    ReplyDelete
  4. ndio hakuna kuleana hapa ameyachagua mwenyewe maisha hayo. alimpiga rungu ray c akimwonya sasa kiko wapi?

    ReplyDelete
  5. Leo umeongea la maana faiza,huu ni ujinga kuwapeti peti watu wazima na madevu mpaka matakoni ambao wameona mifano ila wanataka kuiga ujinga,na kuwapa attention za kijinga kama hizi ndio kunawafanya wengine kufanya huu ujinga,dawa ni kuwakanya Kwa ukali kabisa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad