Ali Kiba Asema Atahakikisha Anafanya Kazi na Master Jay na P – Funk

Staa wa muziki Ali kiba amedai anatamani kufanya kazi na producers wa Kitambo kwenye sanaa Tanzania, Master Jay wa MJ Records pamoja na P Funk Majani wa Bongo records.
Ali Kiba

Akizungumza katika kipindi cha The playlist cha Times Fm, Kiba amesema hakuwahi kufanya nao kazi ndio maana ana hamu nao sana.

“Kiukweli Master Jay na P funk natamani sana kupiga nao kazi, na naahidi kuwatafuta na kufanya nao kazi, kwa hiyo fans wangu wategemee kazi nzuri ntakazofanya nao” alisema.

Katika ‘line’ nyingine King kiba amedai, anamkumbuka sana pia producer aliyetengeneza kazi zake kadhaa, KGT kwa sababu alikuwa ni zaidi ya mwalimu wa muziki kwake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad