Baada ya Chama Cha Walimu Kukosoa Mpango wa ‘Daladala za Bure Kwa Walimu’ Dc Makonda Kawajibu Hapa

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda Jumapili ya February 28 2016 alitangaza kuwa Walimu wa shule za Dar es salaam wataanza kupanda daladala bure kuanzia March 7 2016 baada ya kukubaliana na wamiliki pamoja na madereva wa daladala, habari hii wengine wakaipokea vizuri wengine wakaikosoa.

Dc Makonda amehojiwa na millardayo.com na kusema ‘Najua nipo kwenye jamii ambayo inapenda kuongea sana kuliko kufanya kazi, jamii inayojua kuongelea kukwama kwa jambo hata kabla ya kuanza kufanya kazi , watu wengi wanesema tungewapa pesa ya nauli, wengine wanasema pesa hizi wangepewa wanafunzi, wanasahau kama Walimu ndio uti wa mgongo wa taifa‘

‘Huu ni mchango wa wadau, wadau ndio wanawasaidia Walimu, mimi nasimama kama daraja tu na inabidi watu wajue huu sio mpango wa serikali, ni wadau wamekubali kusaidia Walimu, watu wasichanganye mambo, Mkuu wa Wilaya hana pesa‘ – Makonda
‘Nadhani Walimu walitakiwa kwanza kushukuru wamekumbukwa, ningefurahi wangesema tumepokea nafasi ambayo jamii sasa imeanza kutambua heshima ya Walimu, kwa moyo huu ambao Wadau wameuonyesha tunaiomba sasa wizara ya elimu iendelee kuangalia kuboresha zaidi‘ DC Makonda

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. DC Makonda anastahili kuliangalia upya. Jambo hili lina mambo mengi. Acha uwezekano wa walimu kudhailika katika mpango huu lakini anahitaji kujua kuwa yeye ni DC wa Kinondoni na si DC wa Walimu wa Kinondoni. Madaktari na manesi anawaambiaje? Wafanyabiashara nao je anawaambiaje? Wote hulipa nauli. lakini na magari yatokayo kibaha yakikutana na walimu yanapoingia eneo la Kinondoni yafanyeje? Au walimu wanaotoka mkoa wa Pwani kama Kibaaha wakipanda wafanyeje magaru waliyopanda yakiingia eneo la 'nafuu ya nauli'. Amekuwa na haraka bila kulichambua jambo lenyewe kwanza.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inasikitisha sana unapotolewa msaada wa kujitolea unakuwa na maswali ya siyo na majibu jiulize wewe umefanya nini ktk kusaidia jamii sio kujitia fundi wakudodosa na viji swali mshezi ndo nyinyi mliokosa shukurani hata unapofadhiliwa unaona ni jukumu la mtu akukusaidie kukupa hata bure usitoe shukurani

      Delete
    2. Ukipewa utaomba na mama je akipewa mama utasema na mjomba je na dada mbona hajapata binaadamu hatuna shukurani

      Delete
  2. Mh. DC kama kweli anataka kuwasaidia Waalimu ajenge hoja waalimu wapewe posho ya usafiri. Hapo itakuwa safi kabisa.

    ReplyDelete
  3. BRAVO MR. MAKONDA. HIVYO VITAMBULISHO WACHUKUE WALIMU WATAKAO PENDA KUCHUKUA, SIO LAZIMA NA WALA HAWALAZIMISHWI. ASIYETAKA KUPANDA BURE NA ALIPE NAULI YAKE KAMA KAWAIDA...........SHIDA IKO WAPI HAPO?? MSITAKE KUMCHOSHA WALA KUMKATISHA TAMAA MUHESHIMIWA MAKONDA.....DUH!! YAANI WAPINZANI MNAPINGA MPAKA MAJINA YENU....HAPA KAZI TU!!

    ReplyDelete
  4. Hao walimu waliomba huo msaada au kiherehere cha panzi? Unatafuta ujiko kwa nguvu? Kinondoni tu ndio kuna walimu? Au ealimu wanaofanya kinondoni lazima wanaishi kinondoni? Anayrishi ilala na kufundisha Kino inakuwaje hapo. BULL SHIT

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anony 3:30 PM usiwe mburura kwani ilala hawana DC kila mmoja ana mipaka yake kikazi

      Delete
  5. MAUJIKO ANATAFUTA JAMANI!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad