Uchaguzi wa Meya Dar es salaam unazidi kuchukua headline kila siku. Ikiwa jana tu Baadhi ya Wabunge na Madiwani wa Ukawa walitinga ofisi ya Halmashauri ya jiji kutaka kujua tarehe ipi uchaguzi utafanyika lakini hawakupata majibu hayo. Leo March 5 2016Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA‘ Taifa, Freeman Mbowembele ya Waandishi wa habari ameyazungumza haya….
’Hatutaomba tena kumpata Meya wa jiji la Dar es salaam, tutadai kumpata Meya, Serikali wasifikiri watapanga wao tarehe ya kumchagua Meya, wamekuwa na utaratibu wa kutaka tarehe ya kumchagua Meya kwa kutushtukizia masaa 24 kabla, kanuni inadai siku saba, tutataka tarehe ya kuchagua na siku hiyo atachaguliwa Meya asipochaguliwa Meya siku hiyo tusilaumiane’:-Freeman Mbowe
Aidha Mbowe ametoa msimamo wa chama alipoulizwa kama watasusia uchaguzi, haya ni majibu yake…
’hatuwezi kususia uchaguzi wa Meya kwa sababu ni haki yetu kuongoza jiji kwa sababu ni maamuzi ya wananchi kwa hiyo hatuwezi kususa maamuzi ya wananchi’:-Freeman Mbowe
uchaguzi wa meya shida hivi wa ccm watakubali kutoa nchi kweli
ReplyDelete