Baba wa Mwanamuziki Diamond Platnumz Ashinda Njaa Huku Mwanawe Akitumbua Mil 100 Ujerumani....

Wakati mwanaye staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na mwanaye Tiffah wakiteketeza kiasi cha fedha kinachokadiriwa kufikia  shilingi Mil.100 barani Ulaya walikokwenda kula bata, baba mzazi wa msanii huyo, Abdul Juma anadaiwa kushinda njaa kutokana na ugumu wa maisha, twende na Risasi Jumamosi.

Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mzee Abdul Juma.
Diamond na familia yake hiyo sambamba na madansa wake, waliondoka nchini mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda Frankfurt, Ujerumani ambapo pamoja na kufanya ziara ya kimuziki katika nchi tofauti balani Ulaya, staa huyo aliitumia ziara hiyo kuponda raha.

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ pamoja na mtoto wao Tiffah wakila ‘bata’ Ulaya.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kililiambia gazeti hili mapema wiki hii kuwa, baba Diamond kwa sasa ana maisha magumu na mara nyingi amekuwa akishinda njaa huku baadhi ya majirani wakimpa msaada hali inayowasababisha kushangaa baada ya kusoma kwenye magazeti kwamba mwanaye huyo anatumbua fedha kibao na familia yake, ndugu na marafiki huku mzazi wake huyo akiteseka.


“Jamani baba Diamond anateseka! Muoneeni huruma. Alikuja kwangu kuniomba elfu moja lakini bahati mbaya na mimi sikuwa nayo. Mara nyingi amekuwa akishinda njaa. Mbaya zaidi anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu na hana mtu wa kumpeleka hospitali. Njooni mumuone yupo hapa  kwake anatia huruma,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Kiukweli baba Diamond anasikitisha sana. Tunashindwa kujua tatizo liko wapi kati yake na mwanaye, maana kuna wakati huwa anamsaidia lakini wakati mwingine anampotezea.”

MAPAPARAZI WAMUIBUKIA
Baada ya kuzipata habari hizo, mapaparazi wetu walifika nyumbani kwa baba Diamond, Magomeni ya Kagera jijini Dar na kumkuta nje ya nyumba yake akiwa ameshika tamaa huku akionesha hali ya kunyong’onyea kama mtu aliyekata tamaa ya maisha.



HALI YAKE NI MBAYA

Akizungumza na gazeti hili baada ya salamu, baba Diamond alieleza kwamba bado hali yake ya miguu ni mbaya kwani anatembea kwa kuburuza laiti angekuwa kama zamani angeweza kufanya shughuli ndogondogo za kujipatia kipato angalau apate fedha kwa ajili ya kula hasa katika kipindi hiki ambacho hana msaada.

“Niko hapa bado mambo siyo mazuri, miguu inanisumbua kama unavyoona. Nasikia mwanangu (Diamond) ana ziara nje ya nchi na juzi niliona mmeandika ameteketeza milioni 100  na familia yake, namsubiri akirudi huko naamini atanisaidia angalau fedha hata ya kwenda kwenye matibabu na kula kama ataamua maana alishawahi kuniahidi, hali yangu siyo shwari nabangaiza tu hapa,” alisema baba Diamond.


DIAMOND ASEMAJE?

Alipotafutwa Diamond aliyeko Ujerumani kwa sasa ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema hana cha kuzungumza kwa sasa.
“No comment kwa sasa, subirini nikirudi tutaliongea hilo kwa kirefu,” alisema Diamond.

ALIOKWENDA NAO ULAYA
Katika gazeti lenye udugu wa damu na hili, Ijumaa Wikienda la Jumatatu iliyopita, ukurasa wake wa mbele lilikuwa na kichwa kisemacho; DIAMOND
ATEKETEZA SH. MIL 100 ULAYA.

Katika habari hiyo, Diamond aliandikwa kusafiri na ‘ujumbe’ mrefu wa idadi ya watu 14 ambao wote walikuwa chini yake kwa malazi na chakula. Watu hao ni Zari, mama yake mzazi, Tiffah (mwanaye), Romy Jons (DJ wake), Kifesi (mpigapicha), Salam (meneja), mke wa meneja wake mwingine Batu Tale, madansa wanne na dada mmoja ambaye ni ndugu wa Zari. Hao walikwea pipa na kufikia Frankfurt, Ujerumani.

BABA DIAMOND AMEFIKAJE HAPA?
Baba Diamond anadaiwa akiwa angali kijana, alitengana na mama Diamond akiwa na mtoto huyo mdogo kwa miaka mingi bila kumpa huduma zozote kitu ambacho kimemsukuma Diamond kuwa na chuki na ashindwe kumpa matunzo mzazi wake huyo baada ya kupata mafanikio.
Hata hivyo, mara kadhaa Diamond amekuwa akimsaidia fedha baba yake huyo lakini si kwa asilimia mia moja kama anavyomtunza mama yake ambaye anaonekana kula raha hususan kipindi hiki ambacho bwana mdogo huyo kutoka Tandale, maisha yamemnyookea.

Tazama Video Hapa:

Chanzo:Risasi

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hpa tatizo lipo, hakuna alie mkamilifu chini ya jua, diamond amsaidie Baba yake,ila Kuna tabia ya akina mama wengi kupandikiza chuki kwa watoto ili wasaidiwe wao tu

    ReplyDelete
  2. wewe baba Diamond ulimsaliti Diamond wakati akiwa mdogo tena kwa miaka mingi hata hukumtolea msaada wowote wa chakula hata hukumsomesha leo Diamond anao uwezo ndiyo unamkumbuka hata kama akitumia milioni 100 na mama yake mama Diamond anastahili kwa kuwa alimlea Diamond peke yake mpaka alipo sasa hivi, mimi mwenywewe mama yangu alinisaliti nikiwa mdogo kwa muda wa miaka nane niliishi kwa ndugu baada ya miaka nane akaja kunichukuwa leo hii nimeshakuwa mimi na yeye hatupatani hata kidogo, naishi peke yangu kwa kujitegemea mwenyewe, yeye mama siji kuongea nae tena katika maisha yangu sababu aliponiacha niliteseka sana, kwa hiyo Diamond naweza kumuelewa kabisa

    ReplyDelete
  3. Hivi kinachoendelea hapa ni baba kujidhalilisha ama mtoto kumdhalilisha baba? Nashindwa kuwaelewa wote (baba na mwanawe) Baba angeamua tu kukaa kimya ili kulinda heshima yake.

    ReplyDelete
  4. mzee kweli walala na njaa? kuwa muwazi father!!

    ReplyDelete
  5. mzee anataka mteremkoo tuu hana lolote

    ReplyDelete
  6. Alale tu kwani wanao lala njaa si watu kama yeye,,,,

    ReplyDelete
  7. kwani lazima Diamond akusaidie kwani hauna ndugu wengine wa kukusaidia? Wewe mwenyewe ulimsaliti akiwa mdogo bila hata kumjali Diamond na mama yake leo hii unakuja kulalamika eti akusaidie ja asingekuwa na uwezo ungemlalamikia nani? Unataka watu wakuonee huruma hakuna mtu wa kukuonea huruma uliyataka wewe mwenyewe ulipomuacha akiwa mdogo tena mtoto ulitegemea nini? kama leo hii Diamond asingekuwa tajiri wala usingemtafuta

    ReplyDelete
  8. dawa yake hioyoo iamfaaa wababa wengi wasengee wanajifanya wajanjaaa nakuacha wamama wanahangaika na watoto..safi kabisa diamond hakuna kumpa pesa alikuacha ukapata shida leo anakujuaa mamaeee

    ReplyDelete
  9. Nyie mnaomtetea hamjielewi, laiti kama mngejua wababa wa hivyo wanavyonyanyasa wakiwa bado na uwezo wao mngekaa kimya, ninavyokwambia hapa nilipo mume wangu wa ndoa ameondoka nyumbani miaka 7 iliyopita hajui watoto wanakula nini wanavaa nini wanasoma vipi kwa ujumla hajui chochote kinacho husiana na familia ameondoka mtoto wa kwanza yuko std 6 leo yuko chuo, wa pili alimuacha std 4 leo yuko IV nashukuru nina kibarua changu na kibanda jiulize ningekuwa mama wa nyumbani ingekuwaje na maisha yalivyo magumu na aliondoka kwa kisingizio eti anakwenda kufanya biashara ameoa huko huko sumbawanga hadi leo hajatia mguu nyumbani hata kuuliza watoto hawajambo, hata wakimpigia simu hapokei hivi unatarajia nn baada ya hapo, wababa jifunzeni hata kama umemchoka mwenza wako kumbuka watoto kuweka upendo baina yako na watoto wako, ili kuepuka vitu kama hivyo. simlaumu diamond kabisa ni sawa tu akiweza kumsaidia sawa na kama hajisikii basi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad