Breaking News: Balozi Juma Mwapachu Atangaza Kurudi CCM, Adai Alilewa Mahaba ya Lowassa na Ahadi ya Kuwa Waziri wa Mambo ya Nje


HOTUBA YA BALOZI JUMA MWAPACHU KUTANGAZA KUREJEA CCM​


MIKOCHENI 16/03/2016​


Ndugu zangu,

Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba 2015, nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yangu ya uanachama kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni. Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo hayo pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook). Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima haki ya kugombea mcha mungu Edward Lowassa. Nikasema Edward Lowassa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la Watanzania. Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edward Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe Magufuli.

Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowassa, nililewa ahadi ya Lowassa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowassa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.

Leo natangaza kurudi CCM kwa sababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye. Nilihama kwa kwa sababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi kwa sababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama. Usemi wa CCM kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana yake. Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.

Naomba mnisamehe kwa kulifanya jambo langu la kujitoa CCM na kurudi CCM kuwa jambo la kitaifa ukizingatia kwamba sikuwa na nafasi yoyote ya uongozi wa CCM wakati nahama na pia sijawahi kuwa hata Mjumbe wa NEC ya CCM na nilikuwa nje ya ulingo wa siasa za CCM kwa miaka 20. Niliamua kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwa sababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.

Naomba radhi kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14 Octoba) na kutumia msiba wake kutoa kauli za kisiasa zidi ya chama chake alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa mwanachama.

Wananchi wote tumuombee Magufuli na tumsaidie kwani tumepata Nyerere mpya.

Mungu Ibariki Tanzania
mungu Ibariki Afrika

Balozi Juma Mwapachu
Tags

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndumila kuwili Balozi Mwapachu..tutajie umuri wako kabla ya yote Na jipu uliloliweka kwa kidokeza cha nini Na wenzangu!! Kina nani? Je hao wenzako unaodai walikuwa Ni makada wetu? Ktk chama chetu? Naimba hayo majibu Ili tutafakari hatua inayo stahili kukuchikulia wewe.. Magufuli hukuwa. Na imani naye toka ulivyokuwa ATC Na mkafilisi Na hutokuwa. Na imani naye cc baada ya kushika mlichokuwa hamtaki ashike!! We Na hao wenzako mliotaka kutufifizia chama.. Bwana sifiwe.... Allah Akbar... Nangoja majibu yako mh Balozi mstaafu... Hapa Ni kazi tuu

    ReplyDelete
  2. hahahahaha
    ulikurupuka mzee mwapachu
    karibu kwenye ccm mpyaaaa
    hapa kazi tuu
    Mungu mbariki JPJM
    Mungu ibariki TANZANIA

    ReplyDelete
  3. sindio unafiki huo sasa unarudi ili iweje? unadhani magu atakupa cheo? pole kwa kujidhalilisha mbele ya watanzania

    ReplyDelete
  4. uchu wa madaraka mzee! rudi tu ccm na mashabiki watakupoke kama walivyokupokea mashabiki wa ukawa! siasa ya hii nchi ni ya maji taka. kwanini usiwe raia wa kawaida achana na siasa. mashabiki ndio wenye kelele kuliko wachezaji.

    ReplyDelete
  5. Ni zaidi ya malaya,,

    ReplyDelete
  6. Wewe barozi juma mwapachu. Kwa mtazamo wangu usisingizie chama au utawala bora unaonekana wala hauko kwenye utawala bora. Bali upo kimaslahi zaidi ya kupata position ya uongozi wa juu ili kulinda maslahi yako na wala hauko kikazi zaidi bali una lako jambo. Na ndio maana yamekushinda. Kama ilivyodai mwenyewe ulipoona mafiriko ya Lowassa ukajua kabisa ulaji ndio huu tena na huyo Lowasa kwa ujinga akakulewesha kabisa yakuwa atakupa cheo cha waziri wa mambo ya nje. Nawe baada ya kusikia ukavurumisha na vumbi lote kumfwata Lowasa upate cheo au ulaji. Inaelekea Lowasa aliwahidi wengi ulaji. Na sio wewe pekee yako. Na hata wafanyabiashara wakubwa ndani hii nchi kwamba wataendelea kuwa mabwanyenye wa nchi na kuwakandamiza maskini looo huyu Lowasa bora alivyo shindwa angezidi tuharibia nchi. Kweli mungu anaweza

    ReplyDelete
  7. Mtu kama huyu Hana mimamo na hafai kupewa ngazi yeyote. Alitegemea cheo Ukawa na sasa anategemea cheo CCM. hana lake la kubuni kujitegemea. Ni mzigo kwa Taifa na ndumila kuwili.

    ReplyDelete
  8. Mwana mpotevu akirudi kwa baba yake hafukuzwi,bali atapokewa kwa kufanyiwa sherehe.ASAMEHEWE!KARIBU KUNDINI MZEE.

    ReplyDelete
  9. Ndumila kuwili Balozi. katika mtaa wetu tuna nyumba tisa na kiwanja kitupu kimoja.. sasa ushauri Wangu kama bado una umri unaostahili madaraka ambacho ni udhihirisho wa kurudi kwetu ccm.. karibu ila ufamye mitigation kupata hicho kiwa njaa cha kumi ujenge na halafu tutakukarimu kukupa ubalozi wa majaribio kwa mtaa.. na cheo unachokipenda KITAITWABALOZI WA NYUMBA KUMI KUMI..JE UKO TAYARI MWANAPACHU. ...DEAL HILI.. HAPA KAZI TUTAKOMA. .JPJM NI MCHAPAKAZI...UTARIPORI KWA KIJANA PAUL MAKONDA

    ReplyDelete
  10. Ndumila kuwili Balozi. katika mtaa wetu tuna nyumba tisa na kiwanja kitupu kimoja.. sasa ushauri Wangu kama bado una umri unaostahili madaraka ambacho ni udhihirisho wa kurudi kwetu ccm.. karibu ila ufamye mitigation kupata hicho kiwa njaa cha kumi ujenge na halafu tutakukarimu kukupa ubalozi wa majaribio kwa mtaa.. na cheo unachokipenda KITAITWABALOZI WA NYUMBA KUMI KUMI..JE UKO TAYARI MWANAPACHU. ...DEAL HILI.. HAPA KAZI TUTAKOMA. .JPJM NI MCHAPAKAZI...UTARIPORI KWA KIJANA PAUL MAKONDA

    ReplyDelete
  11. Mbona wengi tutarudi,TENA KIMYAKIMYA.

    ReplyDelete
  12. Mwapachu wala isiwe tabu. mimi ninao kuku wawili. mmoja jike na mwingine dume. njoo tusaidiane kuzichunga tuzalishe mtaji ili tufikie ngombe tuanze kuchunga. .wewe na siasa achia ngazi kama kina Samuel sitta. .magumu like anafanya yake ya uhakika na yanaridhisha. .mimi na wewe tumeshachoka na hasitah I mtu anayevurunda. .nakuogopea ww..THIS IS LEADERSHIP NEW ERA. PUMZIKA NJOO TUCHUNGE KABLA YA TRA HAWAJAKUTEMBELEA. .BARIDI

    ReplyDelete
  13. Mwapachu wala isiwe tabu. mimi ninao kuku wawili. mmoja jike na mwingine dume. njoo tusaidiane kuzichunga tuzalishe mtaji ili tufikie ngombe tuanze kuchunga. .wewe na siasa achia ngazi kama kina Samuel sitta. .magumu like anafanya yake ya uhakika na yanaridhisha. .mimi na wewe tumeshachoka na hasitah I mtu anayevurunda. .nakuogopea ww..THIS IS LEADERSHIP NEW ERA. PUMZIKA NJOO TUCHUNGE KABLA YA TRA HAWAJAKUTEMBELEA. .BARIDI

    ReplyDelete
  14. Hivyo Mwapachu unasema uliandika ktk fesi buku ( wewe toka lini na fesi buku?) Hii ni mitandao ya jamii.. we uliihama jamii kufata masilahi sasa umeona rongi namba unajitia kumsifu JPJM na kumkashifu swahiba wako Lowassa 9 ambayo ilikuwa siri yenu(hatuyajui.. leo imeiweka hadharani kinaga ubaga!! sisi tukuamini wewe.. hivyo awamu gani ilikupa ubalozi bila kukujua uzalendo wako na tabia yako hii.. je sisri zetu ngapi za nchi uliuza wewe ktk huo wadhifa tuliokuamini... Maswali ni mengi Ndumila kuwili wewe Pumzika uchunge nini? .... Itabilidi tukupeleke panapo husika akiwemo wa mwanzo swahiba wako lowassa kujibu tuhuma za makubaliano yenu na kujua ulipokuwa kazini uliwajibika vipi na siri ngapi za usalama wa taifa ulizitoa ? Baba hapa ni Kazi Tu JPJM haridhirishwi na haya wala hatokuonea haya kwa haya uliyosema bila Haya!! Mwana kosa HAYA...HAYA SI YETU SISI TUKO TULI NA NCHI INAKWENDA VIZURI NA SALAMA CHINI YA JPJM ... TUOMBE MUNGU TUTAVUKA NA WABADHIRIFU WATAPEPERUSHWA NA MAENDELEO YAKO NJIANI NA UWAJIBIKAJI NA UFANISI ITS CALL OF THE DAY... HAPA KAZI USIENDELEE KUJIUMBUA ZAIDI TOSHA MWAPACHU.... HATUA IKO NJIANI NA TUTAKUHITAJI MUDA SI MREFU UJIELEZE.. HASA ULIPOKUWA UKITUWAKILISHA...NDUMILA KUWILI

    ReplyDelete
  15. Inatisha hii ya Mwapachu.. Balozi Sefue unasemaje hapa.. manake huyu pia ni Balozi... yr comments for way forward. .tumeuzwa

    ReplyDelete
  16. Inatisha hii ya Mwapachu.. Balozi Sefue unasemaje hapa.. manake huyu pia ni Balozi... yr comments for way forward. .tumeuzwa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad