Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mh Godless Lema amefunguka na kusema kitendo kilichofanyika katika uchaguzi wa Halmashauri ya Kilombero leo ni ubabe na uhuni wa CCM.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Godbless Lema amesema kitendo cha polisi kuwakamata wabunge wa Chadema na kuwaweka ndani wakati uchaguzi wa Halmashauri ukiendelea ni mbinu waliyotumia CCM ili kupunguza kura za wajumbe hao, jambo ambalo limepelekea UKAWA kushindwa ili hali wao walikuwa na wajumbe wengi zaidi ya CCM.
"Leo ilikuwa siku ya Uchaguzi Halmashauri ya Kilombero baada ya kuahirishwa mara kadhaa. UKAWA ina wajumbe 20 na CCM 19. Hii ina maana kuwa UKAWA tulikuwa na uhakika wa kushinda na kuongoza Halmashauri hiyo. Baada ya CCM kujaribu kuwahonga madiwani kadhaa na kushindwa kufanikisha lengo lao, leo wakabuni mbinu mpya ya kishetani. Wakamkamata Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali na Mbunge wa Viti Maalum Devotha Minja na kuwaweka mahabusu huku uchaguzi ukiendelea" Aliandika Godbless Lema
Kufuatia jambo hilo Mbunge huyo amesema kuwa jambo hilo ni jambo ambalo halivumiliki kwani ni ukatili, ubabe na uhuni
"Kwa kufanya hivyo wakawa wamepunguza kura 02 za UKAWA (kura ya Lijualikali na ya Devotha). So UKAWA ikabaki na madiwani 18.
Uchaguzi umefanyika CCM wameshinda kwa kura 19 na CHADEMA 18. Huu ni ubabe, uhuni na ukatili usiovumilika. We must take action. Haiwezekani tuhujumiwe kwa kiasi hiki halafu tukae kimya. Huu ni ubabe ambao hata Shetani hawezi kuufanya.
Tusipochukua hatua wataendeleza ubabe huu wa kijinga. Watafanya hivyo pia kwa Dar" Aliongeza Godbless Lema.