CHADEMA Warusha Kombora Kwa Rais John Magufuli...Wadai Wamechoka Sasa


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimerusha kombora kwa Rais Dk. John Magufuli na kusema kuwa sasa wamechoka na uonevu.

Chama hicho kimesema kuwa wanashangazwa na hatua ya kukamatwa kwa wabunge wao huku viongozi wa juu wa Serikali wakibaki kimya, hasa Rais Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

Kimesema tangu ulipovurugika Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, wabunge na madiwani wao wamekuwa wakikamatwa na kudhalilishwa kwa madai ya kufanya fujo jambo ambalo si sahihi.

Akitoa tamko la Kamati Kuu kwa waandishi wa habari Dar es Salaam , Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema katika kipindi cha siku mbili watatoa tamko kwa wanachama wao ikiwamo kuchukua uamuzi mzito kutokana na vitendo hivyo vya udhalilishaji.

Alisema kuwa vitendo hivyo vya uonevu ambavyo vinafanywa na Jeshi la Polisi, vinatokana na shinikizo la viongozi hao wa Ikulu na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mbowe alisema wakati vitendo hivyo vinaendelea, Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue wamekaa kimya, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa wanahusika kutoa amri ya kufanyika kwa vitendo hivyo.

Alisema hadi sasa Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee wamezuiliwa na polisi kwa ajili ya kuhojiwa huku baadhi ya askari wakienda nyumbani kwao kwa ajili ya upekuzi.

Mbowe alisema wakati hali hiyo ikiendelea, hivi sasa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amekuwa akitafutwa na polisi kwa madai kama ya wenzake ya kuvuruga uchaguzi.

Alisema chama hicho hakitavumilia kuona vitendo vya wazi vya kuua demokrasia nchini vinafanyika, na kwamba kikao hicho kitakuja na uamuzi mzito wa kitaifa ambao utawasilishwa kwa wanachama ili kuchukua uamuzi.

Mbowe alisema hawawezi kuvumilia vitendo vya unyanyasaji, uonevu na dhuluma inayofanywa na Serikali ya CCM, hivyo basi watatangaza uamuzi mzito ambao utafanywa na wanachama wao nchi nzima.

“Tumechoka kunyanyasika, tutatoa tamko kali la kitaifa ambalo litawasha moto kwa wanachama wetu, kwa sababu wao wameandaa mkakati wa kuua demokrasia nchini, hatutakubali.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tamko toka mtoe matamko kibi cha maana munapata

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad