CHID BENZ 'Watanzania Wenzangu Siko Sawa Nahitaji Msaada Wenu'


Akiongea kwa uchungu kwenye kipindi cha Da Weekend Chat Show cha Clouds TV jana, Chidi ambaye mwili wake umepungua kwa kiasi kikubwa, amesema bado uwezo kimuziki anao lakini wale aliowaita wadau walioushikilia muziki wamemtupa.

Amesema wakati wa kilele chake, alikuwa akifanya show kila siku katika wiki, lakini kwa sasa mambo yamebadilika kabisa. “Matatizo yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu unapungua kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alisema.

Chidi amedai kuwa kuna watu wanaamini kuwa kama akiwa juu, wasanii wengi wa hip hop watakuwa na wakati mgumu. “Hawa Joh Makini sijui, nani wanakuwa hawapo. Sasa hakuna mdau anayeweza kukubali akina Joh Makini wasikuwepo awepo Chidi Benz peke yake,” alisema.

Katika hatua nyingine Chidi alisema pamoja na afya yake kuzorota, hivi karibuni alipiga show kwa masaa mawili hadi mama yake akalia. "Mama yangu akaniambia mwanangu unafanya show two hours, show kali watu wanapenda unachokifanya lakini sioni mwamko wa watu kutokea kukusaidia, kwahiyo tufanye mpango watu wakusaidie' na mimi namuambia nataka watu wanisaidie, natamani kusaidiwa, natamani kupata mafanikio anayopata Diamond," alisisitiza.

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. "Kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe"

    ReplyDelete
  2. MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI.

    ReplyDelete
  3. Pole Chidi,lakini tusisahau kuna neno linasema utavuna ulichopanda,na hapo wasanii na watu wenye tabia kama za huyu bwana ndio wajifunze.

    ReplyDelete
  4. ACHA KUBWIA UNGA FALA WEWE

    ReplyDelete
  5. Drugs sio dili , wasanii wengi wa bongo ni wakuigaiga tu life style mwisho wa cku zinawatokea puani, ona sasa jamaa alivyochoka😡😡😡😡

    ReplyDelete
  6. Nilimuona chidi sikuamini kama ndiye,nilitamani kumuuliza ana masaibu gani,lakini niliogopa kwa jinsi alivyo mwepesi kutukana au kupiga.Ama kweli dunia tambara bovu,TUMUOMBEE!

    ReplyDelete
  7. MMMMMMMMMMMM!!!!

    ReplyDelete
  8. Huyu chid benz wakati ray c anamshauri mambo ya kweli alimpiga dada wa watu leo ndo anahitaji msaada wa kibinadamu kweli!!! Ama kweli shida haina adabu.

    ReplyDelete
  9. DUUH!BINADAMU HUJAFA HUJAUMBIKA.

    ReplyDelete
  10. Acha sembe baba,Eeh

    ReplyDelete
  11. Mungu atakusaidia na tumuombee yeye hakutaka

    ReplyDelete
  12. Inasikitisha sasa fanya maamuzi anza kuhudhuria clinic za drugs abuse rudi kwa Mola wako ibada muhimu sana hkn kinachoshindikana kikubwa ni maamuzi tu yaani nimeumia sana muonekano wako ulivyo

    ReplyDelete
  13. unataka mafanikio km ya Diamond.inshalla utayapata acha unga na show-off ulozokuwa nazo Diamond is very smart boy achezi na ujinga km wako au yule mpuuzi mwenzio Mr Nice.mafanikio ya Diamond mtayasikia tu na kuyaona kwenye Instragram.

    ReplyDelete
  14. Nakupa pole. Katika dunia hii kuna mambo mawili tu. Nitakutolea mifano: Kuna mtu mwembamba na mnene,mweusi na mweupe,tajiri na masikini, mrefu na mfupi, Mrevi na sio mrevi, mtumia madawa na si mtumia madawa. Sasa wewe uko upande gani. Kupanga ni kuchadua!! Hakuna mtu wa kukusaidia hata kama ni mama yako, baba yako na hata raisi wako. Mtu wa kukusaidia ni wewe mwenyewe. Mungu akubariki na akuongoza katika kuchagua kipi bora na kipi sibora kwa maisha yako.
    Wako JB, USA.

    ReplyDelete
  15. Wee zidi kula unga tu , mwisho wa siku hakuna atakae kusaidia zaidi ya hospitari... hata kama uwezo ninao siwezi kukusaidia mjinga wee,, endeleza majivuno yako tuone sasa!!!

    ReplyDelete
  16. Unasema ni stess ndo zinakumaliza, mbona hujasema unga ndo unaopelekea kufikia hapo??
    Huna ustaaeabu na unajifanya unajua kila kitu.. Mziki wako huwezi kuufikia wa joh making ata kwa dawa so usijifanye ooh sina wadau koz unaweza zaid ya wenzako...hakuna mdau anataka kumsupport teja o else nenda rehab urudi kama zaman na upunguze mashauzi ya kifala uonee wadau tutakavyokusupport.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad