Chama Cha Wananchi (CUF) kilishaeleza msimamo wake kuhusu ubakaji huo wa demokrasia kupitia taarifa yake kiliotoa tarehe 18 Machi, 2016. Baada ya hatua ya jana tunaweka msimamo wetu kwamba:
1. Hatutambui hicho kinachoitwa matokeo ya uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016 na kwa maana hiyo hatumtambui huyo aliyedaiwa kuwa mshindi na kwa msingi huo huo hatutoitambua wala kushirikiana na Serikali itakayoundwa kutokana na matokeo hayo batili ya uchaguzi batili.
2. Tunawapongeza kwa dhati Wazanzibari wote kwa ukomavu wao mkubwa wa kisiasa waliouonesha kwa kuitikia wito wa mpendwa wao Maalim Seif Sharif Hamad na chama chao cha CUF na kutoshiriki katika uchaguzi huo batili. Kwa ujasiri wao huo wameudhihirishia ulimwengu kwa njia za amani na za kistaarabu kwamba chaguo lao ni Maalim Seif Sharif Hamad. Kwa mara nyengine tena Wazanzibari wameyathibitisha maamuzi yao ya kidemokrasia waliyoyafanya kupitia uchaguzi huru na wa haki wa tarehe 25 Oktoba, 2015.
3. Tunavipongeza vyombo vya habari vya ndani na nje na jumuiya ya kimataifa kwa kuonesha hali halisi ilivyokuwa na jinsi Wazanzibari walivyoikataa CCM, walivyowakataa watawala na walivyokataa kutumika kubaka demokrasia. Wazanzibari wameandika historia nyengine mbele ya macho ya ulimwengu. Kwa mara nyengine tena Wazanzibari wameshinda.
4. Tunajua Wazanzibari wana hamu ya kujua hatua zinazofuata katika kusimamia maamuzi yao ya kidemokrasia waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015. Chama chao kinawatoa wasiwasi Wazanzibari kwamba hakijayumba na kinafuatilia haki yao hiyo kwa njia za amani na za kidemokrasia na kitakuwa kikiwaeleza kila kinachoendelea.
HAKI SAWA KWA WOTE
NASSOR AHMED MAZRUI
NAIBU KATIBU MKUU – CUF
22 Machi 2016
Hakuna kukubali kirahisi tupo tayari kwa lolote tushachoka uonevu, haki hata kwa njia ya upanga itapatikana
ReplyDeleteKazi Mnayo subirini 2020
ReplyDeleteCCM WAPUMBAVU
ReplyDeleteCUF hampewi nchi msicheze na hisia za watu mara 5 mnapigwa changa la macho ndo maana Balozi iddi akasema mabwege na kama ni mabwege basi CCM wataendelea kukuibieni ushindi
ReplyDelete1995, 2000, 2005, 2010, 2015 na 2020 tukiwa hai na uzima inshaallah sound zinu zinajulikana mkwala kwenye majukwaa ya kampeni tu. Mliahidi wanachama wenu msipopewa Serikali mwaka huu wa maamuzi mnanganganua, wakowapi hao vidume wa kunganganua.
Bora mvunje chama tu tuendelee na system yetu ile ile ya chama kimoja kwani CCM wanavyosema Nchi hawatoi kwa vikaratasi mlijua wanatani?
Wanamaanisha kwamba mnataka nchi na nyinyi mpindue kama wanavyokupinduweni kila miaka mitano ya uchaguzi.