Daktari Afunguka: Maini ya Penny yameanza Kuharibika Sababu ya Unywaji wa Pombe Kali.....

Habari mbaya! Majibu ya daktari yamemkatisha tamaa Mtangazaji wa Zouk TV, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ baada ya kuambiwa kuwa, kutokana na unywaji wa pombe kali kupitiliza, maini yake yameanza kuharibika na asipochukua hatua za haraka hali itazidi kuwa mbaya zaidi.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Penny, hivi karibuni mrembo huyo aliyewahi kuwa mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alikuwa hajisikii vizuri na mara nyingi alipokuwa akijaribu kula, alitapika na kuishiwa nguvu hivyo akaamua kwenda kupima kwenye Hospitali ya AAR jijini Dar.

Mpashaji huyo alidai kwamba baada ya Penny kuchukua vipimo vyote, ilibainika kwenye maini yake kuna tatizo na chanzo chake ni unywaji wa pombe kali.“Maskini Penny, sasa hivi hana raha kabisa tangu daktari amwambie ana matatizo kwenye ini, mara nyingi anakuwa mnyonge na mwenye wasiwasi sana,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Penny ambapo alizungumza kwa upole kuwa angeomba vitu vingine asiviweke wazi kwenye vyombo vya habari kwani ni mambo ya kidaktari zaidi.

“Kiukweli sijisikii vizuri na hata kuongea sana naona shida. Unajua vitu vya kidaktari siyo vizuri kuviweka kwenye vyombo vya habari. Kifupi sipo vizuri,” alisema Penny akionekana kutokuwa na furaha.
 GPL

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tangu lini daktari akafunguka maradhi ya mgonjwa!! Nyinyi wabongo mna mambo!! PS Kama ni kweli ukiisha ugua ini jipange......

    ReplyDelete
  2. Sasa nyi udaku kuna siri mliyobakiza pamoja na Penny kuwasihi?

    ReplyDelete
  3. na kweli daktari haruhusiwi kutoa siri ya mgonjwa, au kutoboa siri ya mgonywa, na hata kama maini yakiharibika unaweza kutibiwa bila ya kuwa na wasiwasi wowote pia ukipunguza kunywa pombe au ukiacha kunywa pombe kwa muda wa mwezi mmoja maini yanajirudi kwenye hali ya kawaida kwani mimi naishi ulaya nilishapitia kwenye matatizo hayo nikiona nimekunywa sana huwa naacha kwa muda wa mwezi ili maini yajirudi na nikitu kinaweza kutibika. na ukiwa na matatizo ya maini acha kunywa pombe kwa muda wa mwezi mmoja, ndani ya wakati huo kula sana chakula, kunywa maji mengi na matatizo yataisha.

    ReplyDelete
  4. Majuto mjukuu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad