Diamond Platnumz Afungukia Mimba Nyingine ya Zari

STAA wa Bongo Fleva asiyechuja kwa takriban miaka 7 mfululizo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameeleza mikakati yake kuwa ana mpango wa kumpa mimba nyingine malkia wake wa nguvu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Risasi Jumamosi linakuhabarisha.

Diamond ambaye tayari amejaaliwa mtoto mmoja (Tiffah) na mrembo huyo raia wa Uganda, amefunguka jambo hilo hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano mafupi na mwanahabari wetu kuhusu mikakati yake ya kimaisha.

Alisema anamshukuru Mungu Zari kukubali kumzalia Tiffah tofauti na warembo wengine aliowahi kutembea nao lakini kwa kuwa yeye anapenda watoto, ameanza ‘kuchakarika’ ili Tiffah apate mdogo wake na si huyo tu, hata na mwingine kadiri Mungu atakavyombariki.

“Mimi napenda watoto. Bahati nzuri Mungu pia amenipa mwenzangu ambaye naye anapenda watoto. Hivyo si vibaya nikifikiria mtoto mwingine na mwingine yani kadiri Mungu atakavyonijalia.

“Yote hayo nitayafanya kwa utaratibu maana si unajua tena shughuli zangu za muziki nazo zinanibana, bado nahitajika nilee familia hivyo nitajipanga vizuri nina imani hakuna kitakachoharibika,” alisema Diamond.

Kabla ya kukutana na Zari, kwa nyakati tofauti Diamond aliwahi kubanjuka penzini na warembo kama Penniel Mungwila ‘Penny’, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Wema Sepetu ‘Madam’ pasipo kupata mtoto ambapo staa huyo wa Wimbo wa Utanipenda akisema warembo hao hawakuwa tayari kumzalia kwa kile alichodai kuwa walizidiwa na nguvu ya ujana.

Chanzo: GPL

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kuna mtu kamkazata kuzaa? au bado ajiamini anaanza na promo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anajibu alichoulizya na wanahabari.

      Delete
  2. ANAPENDWA KUTAJWA TUU LABDA KATUNZI AMSAIDIE TENA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaa wee yule unaemwita baba alivyosaidiwa na wauza mkaa. Kimaza chako kichangujee. Chupi mkononi kaa yule kura 90. Mbwa usie na DNA wee. Mfyuu

      Delete
  3. Ndoa lini ndguyangu au kuzini ndo fashion

    ReplyDelete
    Replies
    1. we umezn mara ngap ndugu au kaz kunyoshea vdole wenzio unasahau kuwa na ww ni nafsi kama nafsi zngne!.

      Delete
  4. Wote mnaomsaidia kutangaza zinaa mtakuwa nae jahanam

    ReplyDelete
  5. Jiekezee Dada wala usirudi nyuma

    ReplyDelete
  6. kampa kampa kampa tena,....... fasta wafunge midomo.

    ReplyDelete
  7. You have a baby making machine just do it haaah lol

    ReplyDelete
  8. janja ya paka hiyo. ripoti ya DNA si nzuri sasa anaanza kujipanga upya.

    ReplyDelete
  9. My brother daimond bado kidogo utakua kama wife pendeza baba unakunywa maji gani

    ReplyDelete
  10. ZAAA TU MOND MUNGU AKIKUPA WATOTO

    ReplyDelete
  11. Kijana wa Kiislamu unajipanga kuendeleza kuzaa wa nje ya ndoa yaani unafanya zinaa wala moyo haushtuki kabisa .
    Kama unampenda kwanini usifunge ndoa ukahalalisha kabisa what the different .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad