Fatma Karume: Dk. Shein Siyo Rais Zanzibar

MJUKUU wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, amepinga hatua ya kumtangaza Dk. Alli Mohammed Shein, kuwa rais Visiwani, anaandika Pendo Omary.

Fatma Amani Abeid Karume, mtoto wa kwanza wa rais mstaafu, Amani Abeid Karume amesema, “Dk. Shein, siyo kiongozi halali wa Zanzibar. Amewekwa madarakani na jeshi na kinyume na Katiba na taratibu za nchi.”

Amesema, “Rais aliyewekwa madarakani na vyombo vya dola, siyo rais wa wananchi. Rais anayewekwa madarakani kwa nguvu za kijeshi na vitisho, hawezi kuwa rais wa wananchi. Anakuwa rais wa majeshi.”

Akiongea kwa sauti ya uchungu na MwanaHALISI Online, Jumatano wiki hii, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Fatma amesema, “Chama Cha Mapinduzi, kisijidanganye. Zanzibar siyo shwari. Kinachotengenezwa sasa, siyo utawala. Ni muendelezo wa chuki, visasi na uhasama.”

Amesema, “CCM ya Tanganyika, ndiyo inayoiharibu Zanzibar. Wanalazimisha viongozi wasiokubalika na wananchi Visiwani kutawala kwa manufaa yao binafsi.”
Soma mahojiano kamili na mwanasheria huyo mashuhuri nchini, katika gazeti la MwanaHALISI Jumatatu wiki ijayo.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nikiangalia kwa makini maelezo ya fatma karume sioni kama maelezo ya mzanzibari mzalendo halisi mwenye kuitakia mema Zanzibar bali yeye mwenyewe fatma karume ndie mwenye kupandikiza chuki,fitna kwa wazanzibari kwa tamaa ya kukitakia chama mjomba wake Mansouri kaka wa mama yake CUF kushika dola kwa tamaa ya kuendeleza family yao kutawala siasa za Zanzibar. Kila nikiangalia ya maelezo ya fatma karume sioni tofauti na matamshi ya mwamko kikundi kilichopigwa marufuku kutokana na siasa zao za chuki za kuhubiriutanganyika ubara uzanzibari,udini nakadhalika. Yeye anashindwa kufahamu yakwamba katika uchaguzi mkuu wa mwanzo wa Zanzibar kulikuwa na hitilafu kubwa pemba ya kimatokeo kulingana na idadi ya wapiga kura halisi. Wazanzibari tunataka mali zote za wazanzibari zilizochukuliwa na familia yake wakati wa utawala wa baba ake ambapo pia mjomba wake mansouri alikuwa waziri zirudi na kuwa mali ya umma kwani walijibinafsisha kinyume cha sheria. Hapana shaka hata yeye mwenyewe binafsi alinufaika katika kujipatia mali kinyume na sheria kutokana na kuwepo wazee wake hao anaotamani warudi tena madarakani ili aendelee kula raha. kama kumlaumu kwanini hamlaumu babu yake aliasisi mapinduzi ya Zanzibar?

    ReplyDelete
  2. Hunamana wewe majeshi ndo yalopiga kura ? Au babaako jeshi maana na yy kamchagua hunakauli yakusema haya chotara ww na babaako mmeiba mali ngapi za nchi hii mnauchungu na zanzibar nyie jielewe ww dr.shein dio chaguo la wazanzibari

    ReplyDelete
  3. wanazua ugomvi kisha wanakimbilia nje ya nchi wakiacha wanyonge wanauana,uliona wapi wakili akawa mkweli?Kama anawezakumyetea mwizi ambaye ameshikwa akiiba na vidhibiti vipo?TAKUKURU tumbueni jipu hilo ili ijulikane anapewa back up na akina nani,
    Mzee Karume aliingizwa madarakani na vikosi vya uhaini dhidi ya serikali iliyichaguliwa na wananchi,sasa huyu anasema kitu gani?Kwa manufaa ya amani au shari?
    Bora angesema hayo Mh.Jussa ningeamini ni mpambanaji wa kudai demokrasia lakini kwa huyu bibie kwa kauli hiyo anajipalia majanga hasiyoyaweza,Baba yake aliomba Nyerere amlinde na jeshi la Tanganyika,akaulize kwa wazee aelimishwe,halafu katika UMOJA na UTENGANO namuuliza anachagua nini?
    Je tuliozaa na wapemba na waunguja tuwafukuze?maana inaonekana Tanganyika kama adui wa Zanzibar kwa fikra zake finyu.
    WAZANZIBAR WENGI WAMETOKA BARA,WAARABU WALIKUJA TOKA HUKO KWAO KWA KUKIMBIA CHUKI ZAO ZAO NA KUWADHALILISHA SANA WATU WETU,HATUTAKI WATAWALE TENA MILELE!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad