Fella aeleza gharama anazotumia kuwatunza vijana 102 wa kituo chake cha Mkubwa na Wanae


Meneja wa kituo cha kusimamia wasanii ‘Mkubwa na Wanae’ Said Fella ameeleza gharama ambazo amekuwa akitumia katika kuendesha kituo chake.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Jumatatu hii Fella anasema kwa kuwa vijana wanaoishi kituoni hapo ni wengi, ameamua kuwa anawahudumia kwa wiki, hivyo anajua hesabu za wiki pekee kuwamudu kwa kila mlo na matumizi yao binafsi.

“Kwa ujumla huwa nachukua chakula kwa wiki na kwa bahati nzuri wanajipikia wenyewe,” alisema Fella.

Fella anasema aliamua kuwafunza kujitegemea hivyo akaona ni bora wajihudumie wenyewe, hesabu zake kwa wiki ni kiasi cha Sh360,000 ambazo hutumia kwa chakula, nauli za shule kwa wale wanaosoma na matumizi mengine pamoja na nauli kwa wale wanaotoka nyumbani kwao.

Pia alisema kwa kuwa huwa haingii jikoni, bado hajajua hesabu halisi, lakini jukumu la kupika hilo analifuatilia kuhakikisha kila kijana anajifunza kujitegemea na kuwa msaada kwa wengine

“Aslay mwenyewe anapika yaani ni kama watoto waliofiwa na mama yao, kila mmoja ana jukumu la kuingia jikoni na kupika chakula cha watu wote, leo Beka kesho atapika Getu. Yaani wote wanaweza kuamua kuingia jikoni watatu au vinginevyo,” alisema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad