Full Time ya Azam FC Vs Yanga ipo Hapa, Juma Abdul Afanya Maajabu Ajifunga na Kukomboa Goli....

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, vilabu vya Azam FC na Dar Es Salaam Young Africans, vilishuka dimbani kucheza mchezo wao wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Takwimu zinatajwa kuwa Yanga na Azam FC kabla ya mchezo wa leo wamekutana jumla ya michezo 15 kila timu ikiwa imeshinda mara tano na kutoka sare mara tano. Katika mchezo wa leo March 4 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam Yanga na Azam FC zimemaliza mchezo huo kwa sare ya goli 2-2.

Azam FC ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la uongozi dakika ya 11, baada ya beki wa Yanga Juma Abdul kujifunga na baadae kusawazisha goli hilo dakika ya 28, Yanga waliongeza kasi baada ya kusawazisha na dakika ya 41 Donald Ngoma akapachika goli la pili.

Kwa upande wa Azam FC wao walisawazisha goli lao dakika ya 70, kupitia kwa nahodha wao John Bocco ambaye ndio mchezaji anayeongoza kwa magoli ya kuifunga Yanga wakutanapo dhidi ya Azam FC, kwani hilo lilikuwa goli la nane kwa Bocco kuifunga Yanga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad