Halima Mdee Atupwa Rumande......Mahakama Yakana Kuzuia Uchaguzi wa Meya Dar es Salaam Wadai Agizo Lilikuwa Feki

Wakati mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee akilala rumande akihusishwa na vurugu zilizotokea Jumapili wakati uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam ulipokwama, Mahakama ya Kisutu imelikana zuio lililotumika kuzuia shughuli hizo.

Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Januari 23, mwaka huu, lakini uliahirishwa ili kuandaa mfumo bora wa upatikanaji wajumbe kutokana na CCM kutaka kuingiza wapigakura nje ya waliotakiwa.

Ulikwama tena Februari 8, baada ya Halmashauri ya Jiji la Dar kubaini kasoro ya nyongeza ya majina 14 ya wajumbe kutoka manispaa za Ilala na Kinondoni.

Jumapili iliyopita ilikuwa ni mara ya tatu, kukwama tena kutokana na zuio lililosababishwa na kesi iliyofungiliwa na Saad Kimji na Suzan Masawe.

Hata hivyo, zuio hilo la muda la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lililotumika kuahirisha uchaguzi wa meya na naibu meya wa Jiji, uliopaswa kufanyika Februari 27, 2016 limebainika kuwa ni batili.

Jana, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Waliarwande Lema alisema Saad Kimji na Suzan Massawe walifungua kesi Februari 5, 2016 wakizuia uchaguzi wa meya na naibu wake ambao ulipaswa kufanyika Februari 8,2016.

Hakimu Lema alibainisha baada ya kufungua shauri hilo, Mahakama ya Kisutu iliweka zuio la muda ili kesi hiyo ianze kusikilizwa Februari 15, 2016 lakini walalamikaji hawakutokea mahakamani hivyo mahakama ikapanga kusikiliza kesi hiyo Februari 23, lakini hawakutokea pia.

Alisema kutokana na hali hiyo, aliliondoa shauri hilo mahakamani hapo na hivyo zuio hilo likawa limekufa.

Aliongeza kuwa aliyesema Mahakama ya Kisutu imetoa zuio ni muongo na kwamba zuio halali ni lazima liwe na jina la Hakimu pamoja na sahihi.

Kukamatwa kwa Mdee
Katika sakata la jana, Mdee na madiwani wengine watatu walilazwa rumande kutokana na kutuhumiwa kumshambulia Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando

Wanatuhumiwa kufanya kosa hilo baada ya vuta nikuvute kutokea Jumapili iliyopita wakati shughuli ya kuwasaka viongozi hao wa jiji zilipokwaa kisiki kwa mara ya tatu, na CCM kuamua kukimbilia mahakamani.

Hali hiyo, ilizua tafrani kati ya madiwani na wananchama wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) baada ya uchaguzi huo kuahirishwa kwa zuio la muda la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Tafrani hiyo ndiyo iliyosababisha vurugu ambazo inadaiwa kuwa katika purukushani hizo Mdee alimshambulia Mmbando mara baada ya kutangaza kuahirisha uchaguzi huo.

Polisi waliokuwa wanalinda usalama kwenye ukumbi wa Karimjee ambako uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika, walimtoa nje Mmbando.

Akitoa maelezo mafupi kwa waandishi wa habari jana baada ya Mdee kuhojiwa kwa takriban saa sita, wakili wake , Profesa Abdalah Safari alisema mbunge huyo anashikiliwa kwa kosa hilo na atalala rumande.

“Kimsingi nilikuja kumsikiliza akitoa maelezo yake, ameshatoa lakini hakuna ushahidi wowote wa kosa analodaiwa kufanya la kushambulia Theresia,” alisema.

Hata hiyo, Profesa Safari alisema kutokana na kosa hilo Mdee alikuwa na haki ya kuwekewa dhamana lakini polisi wamekataa.

“Mdee angeweza kujidhamini hata mwenyewe lakini wamekataa na kutokana na kosa hili anatakiwa kulala rumande kwa saa 48, zikizidi ina maana atapelekwa mahakamani,” alisema.

Profesa Safari, ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Chadema Bara, alisema mbali na Mdee pia madiwani watatu wanashikiliwa na polisi kwa kosa hilo.

Madiwani hao ni Humphrey Sambo wa kata ya Mbezi, Ephraim Kinyafu (Saranga), wakati hakumtaja jina diwani wa tatu.

Awali wakati mahojiano hayo yalipoanza saa 7:00 mchana, taarifa kutoka kwa mmoja wa makada wa chama hicho zilieleza kuwa Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara pia alitakiwa kufika kituoni hapo kutoa maelezo na anatarajiwa kuwasili leo.

Wakati wa polisi wakimhoji Mdee, wanachama wa Chadema walifika kituoni hapo, akiwapo Ester Bulaya, ambaye ni mbunge wa Bunda Mjini, Esther Matiko (Bunga Vijijini) na Henry Kilewo ambaye ni kanda wa Chadema.

Mapema jana mchana kabla ya Mdee kufikishwa kituoni hapo, ilielezwa kuwa polisi walizingira nyumba yake na kumtaka aende kituoni.

Hata hivyo, mbunge huyo hakutoka hadi alipowasiliana na wakili wake ambaye alienda naye kituoni kwa ajili ya mahojiano.

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tukisema askari wanatumiwa na chama tawala watu wanabisha hy ss oneni

    ReplyDelete
  2. Huy Halima Md anastahil kwend jela kwan hana adabu. Kilasik ni yeye ikiwa bungen wala mtaani ni yeye vurug vurug gapa na pale kuwatus wat bil heshima, wamufungulie mashtaka na kutupwa ndani. Na sijui hao walio mchagua eti awe mbunge wao kwan hawasaidie chochot. Na nafas yak ya ubung icukulie na mtu mwingine.

    ReplyDelete
    Replies
    1. nenda kaichukue wewe tumekupa

      Delete
  3. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  4. Sheria ni msumeno. Huyo Halima alisababisha vurugu na kutoa kashfa ni lazima achukuliwe hatua kisheria

    ReplyDelete
  5. Kweli ww una roho mbaya na huna haya looooo mungu akusamehe bure mana hukijui ukisemacho

    ReplyDelete
  6. Msagaji katupwa jela. Haya asage wafungwa wenzie sasa. Kazi kuvunja ndoa za watu tu.mfyuuu

    ReplyDelete
  7. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  8. Halafu ngozi yake ya uso mbayaaa. Mbunge mzima hajui hata vi creme vya kurutubisha ngozi.! Na hizo nyweke majanga matupu. Hata kama we msagaji Halima. Jiweke soap soap. Looo. Uko locaaal. Unajifanyaga mtemi mbona polisi walivyokufata ulifyata mkia mpaka wakili wako alipikuja ?? Lione kwanza.

    ReplyDelete
  9. Mhhh hayo matamshi mengine tunafikiriaga au ropo tuu

    ReplyDelete
  10. Asiyejua maana usimwambie maana ndo mana division zirooooooooo nyingi nchi hii

    ReplyDelete
  11. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  12. Ikiwezekana Polisi nao wachunguzwe ili waswekwe ndani wenyewe kama inavyofanyika nchi nyingine kusudi waace kutumiwa na Chama tawala . Kazi ya polisi ni kutunza amani na si kuwasweka watu ndani kwa woga wa kisiasa. Magufuli asipoangalia ataangushwa tena na wanaccm kwa hili.Anatunbua majitu na anaacha polisi na chama chake kuvuruga Amani, Demokrasia na kuburuta viongozi hasa Mdee kama wanyama. Leteni heshima Kwa wanawake wenye elimu badala ya kuleta vizuizi visivyo na msingi. Wanaume angalieni ubabe katika sehemu za kazi Kwa Wanawake wenye vipaji. Kwenu inalkuwa kama wake zenu mnaowapiga makofi kwa kuwaonea sababu tu ya ndoa. Ndoa ni penzi na si unnyanyasaji.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad