Hapa Nakuletea Picha na Kinachoendelea Kwenye Mkutano Mkuu wa Chadema wa Kutangaza Katibu Mkuu Mpya wa Chama Hicho...

Mambo yanaendelea vizuri ukumbini mpaka sasa Katibu Mkuu anayesubiriwa kwa hamu kubwa atatangazwa rasmi leo Endeleeni kuwa na subira


#LiveUpdates..

Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe anasema umoja wao ndani ya UKAWA ulisaidia kujenga mtengamamo wa kitaifa tofauti na chaguzi zilizopita.

Mbowe: Usiku Hotel ya gold crest ilivamiwa na polisi wakimtaka Ester Bulaya, viongozi wa Chadema wakapambana na polisi.. Kama umeingia chadema na unaogopa kulala ndan bac umekosea njia.

Mbowe: Sasa uchaguzi ndani ya Chadema utafanyika mwaka 2017, uchaguzi mkuu wa chama ni October 2018..

Mbowe: Migogoro mingi ndani ya Chadema imepelekea kuanguka kwa chama, hivyo itashugulikiwa kwa haraka.

Mbowe: Kuiua Chadema kuna gharama kubwa..

Mbowe: Mchakato wa kumpata katbu wa Chadema kuna mambo yake... Ebu ngoja tuache nitasema badae..

Mbowe: Jambo ambalo hatutalivumia ndani ya Chadema ni swala la rushwa kwani rushwa linagawa taifa, sasa swala la rushwa lililelewa na CCM na sasa inataka kuingia Chadema.

Mbowe amewanyooshea vidole wale wanaotumia mitandao ya kijamii..

Mbowe: Kuna majimbo kama Iringa, Rukwa, Arusha Chadema waliachiwa kwa aslimia mia moja na Ukawa hvyo amewataka wajumbe wajitafakari kwanini wameshindwa kuchukua ushindi wa kutosha ktk majimbo hayo.

Mbowe: Mkutano umeazimia kufupisha uongozi ndani ya Chadema, ili kujipanga na kupata nafasi ya kujianda vyema ktk uchaguz mkuu.

Mbowe: Changamoto zilizopo ndan ya ukawa hakuna haja ya kuyakimbia bali ni kupambana nayo.

Mbowe: Kutukana na kuchafua chama

Mbowe: Waraka wa kukamatwa kwa Ester Bulaya umetoka kwa spika wa bunge.

Wajumbe wamekubali mabadlko hayo kwa kauli moja..

Mbowe: Nawashauri tunapokuwa popote lazima tukatae nchi yetu kugawa vipande vipande. Kama kuna kosa tunalifanya Chadema ni kushabikia kuligawa taifa.

Mbowe: Wanaovuruga Viti Maalum ni wanaume kuliko wanawake.. Wanaume wana interest na viti maalumu kwa kiasi kikubwa nchi hii na kuharbu utaratbu

Mbowe: Watu walidhani kuondoka kwa Slaa chama kitakufa..

Mbowe: Watoto wangu walikuwa wa kula sana maharage, sasa siku moja wakala nyama, jirani akasema umeona Lowassa kaja Chadema.. Lowassa hakutoa hata senti tano kununua chama.




Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad