Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetangaza Machi 22 kuwa ndiyo kitafanyika kikao cha Baraza la Madiwani wa Dar es Salaam kujadili ajenda moja ya uchaguzi wa meya.
Uchaguzi huo umeahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali, ikiwamo zuio batili la mahakama lililowekwa na makada wa CCM, katika Mahakama Hakimu Mkazi wa Kisutu.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene hivi karibuni, alisema zuio hilo ni batili na kuagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kufanya uchaguzi huo kabla ya Machi 25.
Kaimu Mkurugenzi wa jiji hilo, Sarah Yohana alisema jana kuwa uchaguzi huo utafanyika Machi 22 kuanzia saa 4.00 asubuhi ukumbi wa Karimjee.
Alisema maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika, ikiwamo kusambaza barua kwa viongozi wa vyama husika na wajumbe watakaoshiriki kikao hicho