Simba wameshuka dimbani kucheza dhidi ya klabu ya wajelajela wa Mbeya Tanzania Prisons, katika mchezo wao 23 wa Ligi Kuu Tanzania bara. Simba waliingia uwanjani kuhakikisha wanapata point tatu ili waendelee kuwa katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.
Hata hivyo licha ya jitihada kubwa kuoneshwa ndani ya dimba la uwanja wa Taifa na Tanzania Prisons za kuataka kutoa sare, hazikuzaa matunda, kwani Simba ilifanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 kupitia kwa Awadh Juma dakika ya 88. Kwa matokeo hayo Simba anaendelea kuongoza Ligi akiwa na jumla ya point 54 akifutiwa na Yanga aliyemzidi point 3 na michezo miwili.
HONGERA SANA,ILA WENYE NAFASI YAO WAMEREJEA KUTOKA KWENYE MICHEZO YA KIMATAIFA,MTASHUSWA TU.
ReplyDelete