Huu Hapa Ndio Wasifu wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dr.Vincent B. Mashinji

WASIFU WAKE KWA UFUPI.

JINA: Dr.Vincent Mashingi

UMRI: Miaka 43
KABILA: Msukuma

TAALUMA: Daktari bingwa wa binadamu (MMED) na Daktari wa Falsafa (PhD).
ELIMU:

1981 - 1987 Elimu ya Msingi (Shule ya msingi Iligamba)

1988 - 1992 Elimu ya Sekondari (St.Pius seminary)

1992 - 1994 A-Level PCB (Mzumbe High School).

1995 - 2001 Chuo Kikuu cha Makerere (Degree ya Udaktari MD)

2003 - 2005 Chuo Kikuu Kishiriki Muhimbili (Shahada ya pili - udaktari bingwa (MMED Anaesthesiology).

2004 - 2004 Chuo Kikuu Kishiriki Muhimbili (Astashahada ya Utafiti)

2008 - 2010 Evin School of Management (Shahada ya Uzamili (Masters) ya Public Relations (CSR)

2007 - 2010 Blekinge Institute of Technology (Shahada ya pili (Masters) ya Usimamizi wa biashara, MBA)

2010-2010
University of Carlifonia - Anderson School (Stashahada ya Management Development)

2008 - 2008 University of Maryland School of Medicine (Astashahada Human Virology)

2010 - 2016 Chuo Kikuu Huria Tanzania (Shahada ya uzamivu (PHD) ya Uongozi.
UZOEFU WA KITAALUMA,

2001 2002, Daktari wa mazoezi - Intern doctor (Hospitali ya taifa Muhimbili).

2002 - 2003, Mtafiti wa kujitegemea (Freelance Researcher).

2003 - 2005, Daktari (Hospitali ya Taifa Muhimbili)

2005 - 2006, Daktari bingwa (Hospitali ya Regency).

2006 - 2008, Msimamizi wa mradi (Shirika la kimataifa la afya IMA World Health)

2008 - 2016, Mshauri wa tiba (TB and HIV), Shirika la afya la Kimataifa la IMA WorldHealth.

NB:
Msaada kwa wafuasi wa chama chakavu ambao definately watakua wanaona "mapichapicha" kwenye elimu ya Katibu Mkuu mpya wa CHADEMA. Ili kuwasaidia wanaweza kukariri kwamba GS mpya wa CHADEMA ana degree 1, Masters 3, Certificate 2, Diploma 1 na PhD 1.

Dr.Mashingi ndiye Katibu Mkuu wa chama cha siasa msomi kuliko wote duniani. Hapa Mbowe kacheza kama "Messi" na "Ronaldo" kwa wakati mmoja.!

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni candidate bora huyu kama ataandaliwa kugombea Uraisi 2020. ni kijana anayehitaji jaramba la siasa tu huku uraiani, kitaaluma yupo poa na tuachane na ushabiki wa kupenda hata jiwe. Vijana mpo?

    ReplyDelete
  2. Kha!! miaka 43 na ma degree yote hayo hahahahahahahaha huyo mwishooooo kama ni u genius basi huyo ni genius wa kuvuka viwango duh!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad