Huyu Ndiye Wema Sepetu Tunayempenda

Wema Sepetu ni mwanamke maarufu si Tanzania tu bali Afrika Mashariki na ana mashabiki wengi zaidi – #TeamWema. Tangu awe Miss Tanzania mwaka 2006, mrembo huyu ameendelea kuwa kwenye headlines bila kupunguza.

Umaarufu wake ulichangiwa zaidi na mahusiano yake ya kimapenzi na watu maarufu kuanzia TID, Mr Blue, marehemu Steven Kanumba, Diamond na hivi karibuni, mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan. Lakini niseme kuwa uhusiano wake na Diamond ndiyo uliomulikwa zaidi kuliko mwingine wowote.

Ni katika uhusiano wao, jina la Diamond lilivuma zaidi hasa kwakuwa kipindi wanaanza, Wema alikuwa tayari kwenye kilele cha umaarufu, na hitmaker huyo alikuwa ameanza kuikwea ngazi.

Kwa kipindi chote hicho, Wema amekuwa ni brand kubwa. Wema ni mgodi unaotembea. Hii ni kwasababu hakuna staa mwingine wa kike Afrika Mashariki mwenye kundi kubwa zaidi la mashabiki nyuma yake. Ni kundi kubwa ambalo lipo tayari kumtetea na kumpigania katika nyakati zote, mbaya au nzuri.

Kundi hili limeendelea kuwa aminifu kwake hata pale anapoanzisha uhusiano na mtu mwingine. Lilikuwa nyuma yake kipindi yupo na Diamond na hadi walipoachana. Limeendelea kumfuata kipindi ameanzisha uhusiano na Idris kiasi cha kuifanya couple hiyo itengeneze headlines nyingi ndani ya muda mfupi.

Kwahiyo kwa namna yoyote ile, Wema ni brand inayoweza kuingiza fedha nyingi. Japo alitakiwa kuwa mbali sana kutokana na ushawishi alionao, nafurahi kuona kwamba tayari ameigundua thamani yake na kuanza kuitumia. Napenda kumuona Wema huyu wa sasa ambaye akili yake imefocus zaidi kibiashara na kupush brand yake ya lipstick, Kiss by Wema Sepetu.

Napenda ninavyoona anavyotumia nguvu kuisambaza na kutafuta mawakala nchi nzima. Ninachofurahia zaidi ni kuona kuwa anaisambaza hadi Kenya ambako kuna mashabiki wake wengi sana. Lipstick zake zipo katika rangi mbalimbali na kwa muonekano wa picha ninazoziona, zinaonekana ziko poa.

Cha msingi sana mashabiki wake wa kike na hata wanawake wengine tu wanaopenda urembo, wamuunge mkono kwa kununua bidhaa za mzawa. Ni kwa kufanya hivyo ndivyo tunavyoweza kutengeneza mastaa ambao hawaiishi kuwa na majina tu, bali pia wanakuwa na uwezo kifedha. Naamini huu ni mwanzo wa Wema kuliwekea thamani jina lake na kutengeneza bidhaa nyingi zaidi sababu wateja wapo.

Leo ameanza na lipstick, kesho anaweza kuja na perfume, lotion, mafuta na bidhaa zingine kibao. Cha msingi napenda kuona akiendelea na mzuka huu wa kupush brand yake yeye mwenyewe kwa nguvu zote. Ni hivi ndivyo wanavyofanya mastaa wa nje kama akina Diddy kupromote bidhaa zao.

Kwa kufanya hivi na kwa jitihada zake, haitachukua muda mrefu kampuni kubwa kuonesha interest ya kuwekeza mabilioni ya shilingi kwenye brand yake. Huyu ndiye Wema tunayempenda, na sio yule wa drama ambaye mwisho wa siku tumejikuta tukimpa jina The Drama Queen.

Source:Bongo 5

Post a Comment

22 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Go go wema we love you

    ReplyDelete
  2. A drama starts all over again

    ReplyDelete
  3. kila mwanadamu anajifunza kutokana na makosa. Tunampenda Wema na wale wanaomtusi moyoni wanamkubali.

    ReplyDelete
  4. MOLA AZIDI KUKUFUNGULIA KILA LA KHERI WEMA. WE ARE PROUD WITH YOU.

    ReplyDelete
  5. tuliza akila Wema fanya maisha yako yawe mazuri. kua mfano wa wasichana wengine, anachana na maneno ya bibi kizee hana jipya bongo

    ReplyDelete
  6. Mungu ni wa wote humpa amtakae kwa wakati wake wanaojiona wako juu wakumbuke watashuka tuu. tunakupenda Wema hata iweje.

    ReplyDelete
  7. mwache Bibi ambemende Kaka sisi tunaendelea na Kisssss by Wema.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndo anaamka sasa?????? wenzake walishaamka siku nyingi sanaa. sasa hivi wanapiga hela vibaya sana mamilioni ya vodacom n.k

      Delete
  8. yes Wema wafunge midomo wanaosema wewe ni fake. ila wamesahau kuonyesha u really wao. opps! bibi nae ni fekizonnnnnnnnnnnn.

    ReplyDelete
  9. kesho mtaona kwenye kiblog cha Sinta atakavyo geuza maneno na kujiita zee la usuzi. kisa aanze kumtukana Wema

    ReplyDelete
  10. Safi wema umefuata ushauri wa ajuza kwamba tangaza biashara yako ya lipstic

    ReplyDelete
  11. Naam umeongea maneno mazuriii huyu ndo wema tunae mpendaaa,ni brand kubwa mnooo afadhali ametambua hilooo mungu ambarik daima

    ReplyDelete
  12. EA sweet heart

    ReplyDelete
  13. ijapokuwa ushakuwa na mahusiano na wanaume wengi,ingekuwa vizuri ukmtafuta mmoja ukafunga nae ndoa, ungekuwa more perfect na Allah angekupa riziki ya mtoto unayemdream. Usijali Allah ni mwingi wa kusamehe,sasa jitambue na umrudie Mungu wako, maisha ya dunia ni ya mapito tu Dada

    ReplyDelete
    Replies
    1. WEWE UMESEMA NENO TULIA UPATE MUME NA MUNGU ATAKUPA WATOTO.UMEJIRUSHA SANA SASA FIKIRIA KUWA NA FAMILIA NA MAISHA YA HESHIMA.

      Delete
  14. Penda Sana wema mwaaaaaaa aaaaah love you so much

    ReplyDelete
  15. Love u my wema from BURUNDI

    ReplyDelete
  16. Love u my wema from BURUNDI

    ReplyDelete
  17. Ayo mambo alitaka kuyafanya toka 2013 ila DIamond ilikuwa anazinguwa.nakumpotezea muda.akamuwa kuchaguwa mapenzi au maisha yake ....akamua kumpiga chini Mond

    ReplyDelete
  18. mpumbavu ameshapitwa na wakati alichelewa atabakia kushabikiwa na malaya wenzake wasio na kazi na elimu ndo wanamshabikia malaya wengi kwenye ushabiki wake hawana kazi.lulu amembwaga lulu mjanja

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad