Imetiamia MBOWE Amtangaza Dk. Vicent Machinji Kuwa Ndio Katibu Mkuu Mpya wa Chadema

DAKTARI Vicent Machinji ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kupitishwa na Baraza Kuu la Chadema, katika kikao chake kilichokaa jijini
Katika Kikao hicho cha Baraza Kuu, Freeman Mbowe alitangaza jina la Dk. Machinji na kuungwa mkono na wajumbe wa baraza hilo, hivyo anajaza nafasi iliyoachwa na Dk. Willibrod Slaa, aliyejienguwa ukatibu mkuu wa chama hicho.

Jina la Dk. Machinji halikuwa miongoni mwa wanachama wa Chadema ambao walikuwa wanatarajiwa kumrithi Dk. Slaa kwani waliokuwa wanatabiriwa kukatia kiti hicho ni Salum Ally Mwalimu, Frederick Sumaye, Benson Kigaila, John Mnyika, Dk. Marcus Albanie na Prof. Mwesiga Baregu.

Nafasi ya Katibu wa Chadema ilikuwa wazi tangu Dk. Slaa alipoondoka Chadema muda mfupi baada ya chama hicho kumpitisha Edward Lowassa aliyetokea CCM kuwa mgombea urais wa chama hicho na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad