Jack Cliff Kuhojiwa Gerezani Kuhusu Vigogo wa Unga Waliokuwa Wakimtuma Kabla Hajakamatwa....

Kila kona kimenuka! Ule mkakati wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ wa kuwasaka na kuwatumbua vigogo wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ‘unga’ ili kumaliza mtandao huo, unadaiwa kumfikia Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ ambaye ni modo wa Kibongo na Watanzania wanaotumikia kifungo nchini China kwa kosa la kukamatwa na unga.

Habari za ndani kutoka kikosi maalum cha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maofisa wa Uhamiaji zilidai kwamba, ukiacha nusanusa ya ndani ya Bongo, kikosi hicho kwa sasa kimeungana na kile cha Polisi wa Kimataifa (Interpol) katika kuwahoji Watanzania hao ili kuwakamata waliowatuma.
“Pamoja na kwamba wengine walishahukumiwa kama Jack Patrick anayetumikia kifungo cha miaka sita Macau (China) tangu mwaka 2013 lakini ishu hapa ni kuwataja wale waliowatuma.

Unajua waliofungwa kama akina Jack wakibanwa lazima watawataja wahusika hivyo kazi ya kuwakamata itakuwa rahisi japokuwa ushahidi unaweza kuwa mdogo.

“Ukweli ni kwamba popote alipofungwa au kushikiliwa Mbongo kwa ishu za unga lazima Interpol watamfikia kama ilivyokuwa kwa Jack.

“Sijui kama atakuwa aliwatajia aliyemtuma lakini mhusika atakuwa tumbo joto huko aliko.
“Unajua baada ya kuona ishu inazidi kuwa ya moto, baadhi ya hawa jamaa waliokuwa wanafanya kufuru ya fedha sasa hivi wamefyata. Zile mbwembwe za kumwaga fedha na kuhonga zimekwisha,” kilisema chanzo hicho kikiitaja China kuwa ni nchi yenye wafungwa wengi wa Kibongo wa unga.
Kwa mujibu wa chanzo kingine kilichomtembelea Jack gerezani katika Mji wa Macau hivi karibuni ni kweli mrembo huyo amekuwa akibanwa mara kwa mara kueleza kigogo aliyemtuma.
magufuli_aapaRais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’.

“Sasa kama aliwatajia ni siri yake na wao (Interpol) lakini suala la kuhojiwa aliyemtuma alishahojiwa sana na sasa hivi ndiyo mambo yamepamba moto baada ya Magufuli kuwatangazia vita,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mfanyabishara za nguo kati ya Bongo na China.

Akizungumzia ishu hiyo, mkali wa sarakasi Bongo, Athumani Ford ‘Wabogojo’ anayefanyia kazi zake za sanaa nchini China ambaye huwa anakwenda kumuona Jack mara kwa mara gerezani alisema kuwa ni Wabongo wengi waliokumbana na msala huo ila mrembo huyo ndiye aliyebanwa zaidi.
Alisema kuwa hata yeye alipata taarifa kuwa Jack alibanwa zaidi kwa kuwa hakutaka kumtaja aliyemtuma mzigo huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad