Sakata la Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba na Mdogo wake Mwamvita kudaiwa kupokea rushwa kutoka kwa raia wa Italia, Vincenzo Cozzolino ili wamsaidie kupata zabuni ya ujenzi limechukua sura mpya.
Sauti na jumbe mbalimbali zilizosambazwa na kuwekwa kwenye mtandao na mtu maarufu kwenye mitandao ya kijamii na mmiliki wa tovuti ya U-Turn, Mange Kimambi, raia wa Tanzania aishie Marekani, zinaonesha mazungumzo kati ya watatu hao, mwaka 2011. Jana, Mwamvita na Makamba walikiri kuwa sauti hizo ni za kweli.
Muitaliano huyo ambaye anadaiwa kumpa Mange Kimambe ushahidi wote wa mawasiliano kati yake na Ndugu hao, amejitokeza na kuwasafisha akidai kuwa hakuwahi kuwapa rushwa wala kuhusiana na January kibiashara.
Cozzolino ameandika ujumbe akidai kuwa ingawa yeye na Mwamvita walikuwa na uhusiano wa mapenzi mwaka 2011 na baadae kujiingiza katika biashara binafsi ambayo ilipelekea kugombana kwao, hawakumhusisha January kwa aina yoyote katika biashara yao.
“Sikuwahi kumuomba [January] kunisaidia katika biashara zangu. Sikuwahi kumpa fedha. Mara chache nilizokutana naye ilikuwa ni mazungumzo ya kawaida ya kijamii. Nilikuwa na uhusiano na Mwamvita. Uhusiano wetu ulikuwa bomba mwanzoni lakini ukawa na mwisho mbaya,” ameandika Cozzolino.
Awali, sauti ya January na mwandishi wa habari iliyosambazwa, January anasikika akieleza kuwa aliwahi kukutana mara moja Dubai na Muitaliano huyo na kwamba alitambulishwa kama mpenzi wa dada yake.
Alisema baadae dada yake alimwambia wameanza kufanya biashara ya kahawa na Muitaliano huyo na baadae biashara hiyo kufa huku ikiwaacha katika mzozo.
Kwa mujibu wa Kamamba, Muitaliano aliyekuwa ameweka nusu ya mtaji ambayo ni dola milioni 50, alianza kudai kiasi hicho cha fedha na sio vinginevyo.
Alisema kuwa awali, muitaliano huyo alikuwa anajaribu kumshawishi Mwamvita amkutanishe na viongozi wakubwa wa serikali ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu.
Hata hivyo, Mange Kimambe ambaye ndiye anayeeleza kuwa na nyaraka zote za ushahidi aliokabidhiwa na Muitaliano huyo na kwamba hivi sasa Muitaliano amelipwa na kukubaliana kumsafisha Mbunge huyo wa Bumbuli.
Mange amesisitiza kuwa ana ushahidi wote wa January na dada yake kupokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara huyo na yuko tayari kuwakabidhi Takukuru.
January Makamba Hatihati Kutumbuliwa Jipu Kwa Ufisadi......Mange Kimambi Aapa Kupeleka Ushahidi TAKUKURU
5
March 07, 2016
WEWE KIMAMBI USIWE MTU WA KUTAKA SIFA ZISIZOELEWEKA AU UMAARUFU KIMAVI,,,, baba yako alikua fisadi na moja katika watu waliokua na makampuni ya famigation tanzania na alikua ananunua tenda karibu nusu ya tanzania. Na ameshafilisi halmashauri za mikoa na wilaya kibao na ndio ukapata kufuta ujinga jaribu unapokomalia mtu kuwa na ushahidi na sio visasi na watu kumbuka marehemu leo angekuwapo mahakama ya mafisadi angekua wakwanza, Sina zaidi ukitaka nielezee ni halmashauri ngapi ntakutajia na mpaka wakurugenzi wa wilaya. Na ma ded wao ninao ukitaka mpaka LPO za kampuni ya baba yako naweza kuzianika humu kwakua ni muhifadhi vifaa mkoa fulani tangu enzi hizo jaribu kuheshimu watu nasio kuona unajua kuliko wote toa ushahidi na sio kuimba tuuuu nimekuchokaq
ReplyDeletekwahiyo wewe unamaanisha kwa kuwa baba yake alikuwa fisadi ndio sababu ya yeye kuogopa kuwataja mafisadi wengine ambao bado wanaendeleza ufisadi..kweli we ndiyo boya unatetea ujinga fala we! peleka kuzimu mambo ya kina marehemu hapa kazi tu. mange songa mbele.
DeleteMange mzushi na mbabaishaji jana nimemuuliza maswali umeshindwa kujibu na umegoma kupost maswali hewani.january amejibu hoja tumesikia tunataka wewe uonyeshe au prove hizo allegation zako sio story tu za kutafuta kick na kuchafuana.wewe mbona ulikimbia dar na kupanda ndege nairobi tueleze shida ilikuwa ipi mpaka ukakimbia then kuhusishwa kwako na drugs mbona upendi kujibu.?chuki binafsi acha the investigation journalist or blogger goes beyond na kama unachofanya wewe take example of assange talk with evidence sio maneno kuwa ulaya halafu bado una tabia za kiswahili tandale ni aibu.be reasonable
DeleteSasa kama baba yake alikuwa fisadi. Ndio iwe sababu ya kulea ufisadi. Nyie mnaishi vizuri wengine wanangaika mnaona maisha yamekula kwenu basi. Hii Nchi ni ya wote. Hamna masikini wala tajili. Mkajambee huko. Hingera sana binti kimambi. Hatuko kwenye enzi za utawala wa mkoloni na wala hatutaki ukoloni mambo leo. Swaihini wakubwa hawaa. Kunyanyasa wenzao tu. Utafikiri wakoloni au ikoloni mambo leo?
ReplyDeleteYaani hii Tanzania kuna mijitu pumba sana. Sasa jitu linamtetea huyu makamba. Hata kama wamearibu sijui limeaidiwa chochote ndio na povu linamtoka hapa. Hawa watu hawafai kwa tarifa yenu ni kampuni ya mufirisi. Watu kama hawa wakipewa uongozi mnashangaa mnamka asubui mnatimuliwa tokeni masikini wakubwa mtupishe matajili kumbe wamesha tia cha mfukoni kwenye mifuko yao hatariiiii na ni shidaaaaa yanatokea haya sio ya kuyafurahiaaa
ReplyDelete