Je Linah Sanga Amewahi Kutoa Rushwa ya Ngono? Majibu yako Hapa

Kipindi cha Enews kinachorushwa na East Africa Television kilitaka kufahamu kama kuna ukweli wasanii hao wa kike huhonga ngono ili wafanyiwe kazi nzuri kwenye hizo kampuni kubwa, Linah Sanga ambaye hata yeye amefanikiwa kufanya videos na waongozaji wakubwa wa video barani Afrika akiwepo Godfather alikuwa na haya ya kusema.
"Sijui kama ipo hivyo sababu mimi kama msanii wa kike sijawahi kufanya kitu kama hicho, kwa hiyo sidhani kama hicho kitu ni cha kweli kwa sababu ukifuatilia kwa wasanii wakubwa wa kike ambao tumeweza kufanya kazi na madirectors wakubwa kama God Father na wengine ni mimi, Vanessa, labda na Aika kwa sasa hivi ambao tayari tumeshatoa kazi zetu, kwa hiyo sidhani kama hicho kitu ni kweli kwa sababu tunafanya kazi na kazi zinalipa ndiyo maana tunaweza kufanya kazi na watayarishaji wakubwa kama hivyo". Alisema Linah Sanga.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. umesema unatamani penzi la Wizkid je yule mganda kaka yake Zari yuko wapi? wakati watu walikuwa wanasema kuwa umeachana na mganda wewe ukasema kuwa ni waongo na wewe na mganda mko poa kumbe hamko poa kakuacha kumbe watu walisema ukweli

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad