Je Unawajua Salama Originals....Kutana Nao Hapa Ujue ni Kina Nani na Wanavyoielezea Kauli Mbiu ya #KuwaOriginal


Bila shaka, mna hamu ya kujua hawa Salama Originals ni wakina nani na jinsi gani wanavyoielezea kauli mbiu ya #KuwaOriginal
1.   Walter Mzengi

Unaweza dhani kuwa ni mmarekani, kama ingekuwa hivyo ingelikuwa ni ngumu mno kwake kujichanganya na washikaji wengine. Huwa anatumia muda wake mwingi akisaka pande tofauti za Dar mahali anapoweza akakuza umahiri wake. Kwa ujumla, kipaji chake kinampa amani na utulivu wa akili wa kufikiri na kutafakari katika maisha. Walter ana maamuzi ya kipekee kuhusu matumizi ya ndomu sababu anaamini kwamba ni rahisi kutumia ili kuzuia mimba zisizotarajiwa na magonjwa ya zinaa kuliko kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa kutotumia kinga.


Yvette: mbunifu wa urembo wa akina dada.

Mwanadada huyu ana bahati ya kuwa na pacha na amethubutu kuwa katika chati akitengeneza mapambo ya akina dada. Kila ubunifu anaofanya hulingana na maumbile ya mteja.  Yeye, anataka kuonyehsa ni jinsi gani msichana ni mrembo akitumia mapambo na anaamini kuwa mwanawake anapaswa kuona uzuri katika mapungufu yake.

Je, una kipaji kilichofichika? Ni muda sasa wa kukionyesha kwa nguvu zote na kufanya kweli. Anza sasa usijejikuta umepoteza muda pasipo na muelekeo.


Rapa Junior

Lengo lake ni kuwa rapa mkubwa. Ni marapa wachache wanachana kuhusu mapenzi, lakini junior yeye amezama kwenye kuchana zaidi kuhusu mapenzi. Ni rapa chipukizi anayeamini kuhusu mapenzi na ni miongoni mwa mambo yaliyo katika mistari yake. Licha ya kurapu, rapa huyu ana kipaji cha kuimba ambapo pia huimba kuhusu mapenzi. Siku hizi, vijana wengi sana wamekuwa wakijihusisha na malavidavi wakianzia sekondari hadi vyuoni. Katika Kuwa Original, kiungo pekee ni kuwa jasiri na kufanya unachokubali. Lolote lile kama ni Sanaa, dansi, muziki hata sayansi unapaswa kuwa jasiri na kufanya jambo hilo sababu una Imani na unachokifanya.


Zuhrura – mshairi

Zuhura ni mwanadada mwenye upeo wa kueleza mawazo yake. Toka sekondari, amekuwa na kipaji cha uandishi. Amekuwa akiandika mashairi yanayoongelea maisha, mapenzi na furaha. Pia, ni mwalimu na kwa sasa anafundisha katika shule ya msingi. Kwa umri alionao, unaweza sema amekubali kipaji chake akiwa bado mdogo. Jambo hili hutokea mara chache, kujikubali uhalisi hasa ukiangalia na hali halisi ya kimaisha. Tumeona vijana wengi sana ambao wamekuwa wakimaliza sekondari bila kujitambua.Kwa Zuhura, ushauri kwake binafsi na kwa wengine ni kamwe kutokuogopa watu wanakufikiria vipi. Fahamu kuwa mafanikio ya mtu yako katika mikono yake mwenyewe.


 Alawi – Dansa

Ni nadra kwa kijana kuwa na kipaji cha kucheza dansi na kuamua kukifanyia kazi. Kutoka kwenye tangazo la Serengeti ambapo alicheza kama Duma mpaka kwenye tangazo la BSS la Salama ambapo alicheza na mwanadada. Alawi yuko vizuri kwenye kazi yake na utashangazwa kwa wigo mkubwa alionao hivi sasa wa kufanya shoo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Pamoja na kipaji chake maridadi bado ametulia. Yupo katika mahusiano na anakiri juu ya umuhimu wa kutumia kondomu na anasema kuwa inawezatokea ukasahau kutumia kondomu, lakini yeye girlfriend wake humkubusha kila wakati. Kuwa makini, cheza karata zako sawa, Mkumbushe mwenzio kutumia kinga kila wakati.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad