JIPU la Uchaguzi wa Meya Jijini Dar es Salaam....Waziri Atoa Amri Uchaguzi Uwe Umefanyika Kabla ya Tarehe Hii....

Hatimaye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene amemaliza mzozo wa uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kuagiza ufanyike kabla ya Machi 25 na kutaja sifa za wapigakura.

Uamuzi huo wa kutangaza tarehe na sifa za wapigakura unaonekana kuwa ahueni kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambavyo vilifurahia hatua kama hiyo, lakini wadau wa CCM wakafungua kesi iliyosababisha uchaguzi huo uahirishwe mara tatu.

Simbachawene, ambaye aliwahi kuagiza uchaguzi huo ufanyike kabla ya Februari 29 lakini ukakwama mara tatu, aliwaambia waandishi wa habari jana mjini hapa kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa kuzingatia kifungu cha 13 (1) cha Kanuni za Kudumu za Jiji.

Alisema watakaopiga kura katika uchaguzi huo ni madiwani wote wa halmashauri za jiji la Dar es Salaam ambazo ni Ilala, Temeke na Kinondoni, wabunge wa kuchaguliwa na wabunge wa viti maalumu ambao mchakato wa kuwapata ulianzia kwenye mamlaka za halmashauri hizo.

Simbachawene alisema wapigakura wengine watakuwa ni wabunge wa kuteuliwa na Rais, ambao ni Dk Philip Mpango, Balozi Agustine Mahiga, Dk Ackson Tulia, Profesa Joyce Ndalichako, Dk Abdallah Possi, Profesa Makame Mbarawa ambao ni wakazi wa jijini Dar es Salaam.

“Tunaomba vyama kuheshimu misingi ya demokrasia kwa kukubali matokeo ili kutosimamisha maendeleo ya jiji la Dar es Salaam,” alisema.



Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. duuu yaaani kwa staili hii kitaeleweka tu. Hapa kazi tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad