Wakati sekta ya usafiri wa anga ikinufaika na kushuka kwa bei ya mafuta duniani, hisa za shirika la ndege la Fastjet zimeporomoka kwa zaidi ya asilimia 35.
Kampuni hiyo imesema kuna uwezekano mkubwa kwa matokeo ya biashara yake kwa mwaka 2016 kuwa chini ya matarajio na kwamba haina matarajio tena ya kuwa na ukwasi kwa mwaka huu.
“Changamooto ya hali ya soko inayoathiri sehemu kubwa ya sekta ya usafiri wa anga barani Afrika, imekuwa ya muda mrefu zaidi ya uongozi ulivyotarajia awali,” taarifa ya Fastjet imeeleza.
Kampuni hiyo, ambayo imesajiliwa kwenye soko la hisa la London, ilikuwa ikitarajia kuhamishia barani Afrika mafanikio ambayo kampuni ya EasyJet iliyapata barani Ulaya. Kwa sasa kuna soko linalokuwa barani Afrika la usafiri wa anga miongoni mwa wananchi wa kipato cha kati.
Fastjet ilianzishwa nchini mwaka 2012, lakini ikasambaa kwenye nchi sita barani Afrika kama Kenya, Zimbabwe na Afrika Kusini. Moja ya nguzo zake ni mfanyabiashara Stelios Haji-Ioannou, ambaye anamiliki EasyJet iliyopata mafanikio makubwa barani Ulaya.
Mwezi uliopita, Stelios alisema hana imani na bodi ya Fastjet na kwamba kampuni hiyo ilikuwa inaelekea kufilisika.
Sir Stelios alitaka mtendaji mkuu wa Fastjet, Ed Winter na mkurugenzi mwingine waondolewe.
“Labda bodi ije na mpango mzito wa kupunguza matumizi, la sivyo kampuni itaingia hasara,” alionya Sir Stelios katika barua aliyomwandikia mwenyekiti wa Fastjet.
Fastjet ilisema imeshasafirisha karibu abiria milioni mbili tangu ianzishwe, ikitoa ofa za bei za chini hadi kufikia dola 10 za Marekani.
Taarifa hiyo ya Fastjet imekuja baada ya mashirika mengi duniani kutangaza faida kwa mwaka 2015. Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga kimesema usafirishaji abiria ulipanda kwa asilimia 6.5% mwaka 2015, ikiwa ni kiwango kikubwa tangu mwaka 2010.
Hata hivyo, Fastjet imesema ina dola 20 milioni kwa mwezi Februari ambazo zitakidhi mahitaji