Katibu Mkuu Mpya Chadema Aleta Taharuki Ndani ya CCM...

Chama cha Mapinduzi kilikuwa kimejipanga vyema kabisa na lundo la tuhuma na kashfa mbalimbali kwa watu kadhaa ambao walikuwa katika list yao kuwa watakuwa wateule wa Ukatibu mkuu wa Chadema.

Habari za uhakika zilizopatikana toka ndani ni kuwa kitengo cha propaganda cha ccm kwa muda wa miezi minne kilipewa jukumu la kufanya kazi hiyo ya kutafiti kasoro za mmoja mmoja kwa wale watu sita ambao wao walisema panga pangua lazima awe mmoja wao.

Kasoro na kashfa hizo zilikwishaandaliwa makala kila mtu na yake ikitegemea nani atatangazwa. Project hii iligharimu fedha nyingi zilizotengwa na chama.

Lakini kitendo cha Chadema kuja na jina geni kabisa kwao ni sawa na kupigwa knock out dakika ya kwanza ya round ya kwanza. Hawakutegenea na wamepigwa butwaa.

Wapo viongozi ambao walikuwa na kikao cha siri hotelini maeneo ya Mikocheni wakisubiri jina litajwe walionekana wakitawanyika usiku wakiwa wameinamisha vichwa chini.

Hata kwenye mitandao ya jamii ambako watu walikesha wakisubiri wachangiaji wengi waliokuwa wanasubiri kuiponda Chadema kwa yale majina waliyokuwa nayo wamechanganyikiwa na kumshambulia Dr Vicent bila mpangilio maana hawamjui.

Chadema kumbe inajua kucheza na siasa za CCM kwa nini haikamati dola kwa mbinu hizi? Hilo ni swali katika mada nyingine

Chanzo: Jamii Forums
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huko ni kuropoka tu bila ukweli wowote. CCM wana mambo muhimu ya kushughlikiwa na hawana muda wa kupoteza kwa kupeleleza ukawa

    ReplyDelete
  2. Muda wanao maana mpaka sasa lowassa bado nihoma ya jiji...umeya ndo huooo waenda ukawa kudadadekiii...lazma mcheue

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante mdau. Mbwa mwitu ovyo kabisa, hawajui hata kupinga baya, mradi limetoka fisiem.

      Delete
    2. ukawa kuna zuri gani
      hamuoni hayaa na uongozi ya meya wenu wa kinondoni
      kazi halijui linaleta siasa

      Delete
    3. Unamzungumzia lowasa yupi, hayo makapi ya CCM au yule FISADI alokashifiwa na chadema nchi nzima??? Leo ndio kawa mzuri kwenu......sema ni homa ya ukawa, sio homa ya jiji,jiji lipi?? Hamumtishii mtu nyau, HAPA KAZI TU, mikwara kwenu......

      Delete
  3. Ni kweli muda wanao km ingekua hivo wangeiacha zanzibar itawaliwe na rais aliechaguliwa kihalali na badala yake wamepoteza muda napesa kwa Uchaguzi wao feki,mfyuuuuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. mtu kashinda kihalali
      ndio ajitangazie matokeo
      zanzibar atutaki utawala wa machotara

      Delete
  4. Kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  5. chadema kwisha habari yao
    znz ccm oyeee

    ReplyDelete
  6. HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
  7. Duh! amakweli akutukanae hakuchagulii tusi. Kwa kitugani hasa alichomzidi Dr. Slaa mpaka alete taharuki CCM??!! Au kwa ile CV aloisifia mbowe kwamba aliongoza mgomo wa madaktari, kwa hiyo haogopi kuua wasio na hatia.......alokutuma labda hukumuelewa vizuri, mkajipange upya......CCM ni ileile, daileee, miaka 8888888888888888888............

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad