Mkali huyo wa wimbo Dar es Salaam Stand Up, anakubalika na vijana wengi kutokana na uwezo wake wa kuandika pamoja na kuchana. Lakini miaka ya hivi karibuni alianza kubadilika baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.
Oktoba 24 mwaka 2014, Chidi alikamatwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere wakati akielekea jijini Mbeya kwa ajili ya show. Lakini kesi hiyo ilimalizika miezi michache baadaye baada ya kuamriwa na mahakama kulipa faini.
Tukio hilo liliwafanya wasanii mbalimbali kuzungumzia hali hiyo huku wakimshauri kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya. Ray C ambaye ni mmoja kati ya waathirika janga hilo ambaye kwa sasa yupo kwenye tiba ya methadone, aliamua kumshauri Chid Benz.
“Pole kaka yangu Chidi Benz. Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitafutia jibu la kutatua tatizo lako. Mimi ni dada yako natumeshafanya kazi pamoja, tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani,” aliandika Ray C kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo Chidi Benz aliendelea na harakati zake huku akijinadi katika vyombo vya bahari kwamba tayari ameshaachana na matumizi ya madawa ya kulevya. Lakini watu wake wa karibu pamoja na marafiki zake walikuwa wanadai kwamba bado hajaacha. Lakini Jumamosi hii akiwa katika kipindi cha Da Weekend Chart Show cha Clouds TV, Chidi amelionekana amechoka zaidi huku akiowamba wadau mbalimbali kumsaidia.
“Matatizo yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu unapungua kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alisema.
Mmoja kati ya wasanii wakongwe wa muziki wa Hip Hop, Afande Selle, alionyesha kusikitishwa na jinsi madawa ya kulevya yanavyomaliza nguvu kazi ya taifa.
“Yanapita kwa njia gani madawa ya kulevya hapa nchini? Anayasambaza nani mitaaani kote mitaani? Madawa ya kulevya hayaleti maendeleoooo,madawa ya kulevya yanaua masela leooooo,” alisema Afande Selle.
Pia wadau mbalimbali wamewataka watu pamoja na wasanii wenzake kumsaidia huku Arnold Kayanda, mtangazaji wa BBC Swahili akisema amelipokea kwa masikitiko suala hilo.
“Kama picha hii ni rafiki yangu Chidi Benz kama nilivyotaarifiwa, kwa hisani yenu wote naomba kila mtu kwa nafasi yake amsaidie. Mimi niko mbali lakini nikirudi nitakutana naye,” alisema.
Licha ya wadau mbalimbali kutaka asaidiwe lakini bado tunaona hakuna msaada wa haraka ambao mpaka sasa umechukuliwa ili kumuokoa Chidi Benz. Serikali ya Magufuli ni sikivu sana, bila shaka kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri kijana mpenda sanaa, Nape Moses Nnauye ataliangalia suala hili.
NABADO MTAISHA JIFUNZEN KWA DIAMOND
ReplyDeleteKuacha kutumia unga ni swala lake binafsi inabidi ajitambue kwamba ana tatizo ili asaidiwe lakini mkimlazimisha atarudi tena kule kule.
ReplyDeleteNaomba hyo chid amuonyeshe hyo anayemuuziaga hyo madawa amtibie mbaka apone na kukamatwa kwkua anaangamiza vijana ndio taifa la ksho
Deleteakifanya kama ray c ndio atasaidiwa, hatutaki kutwanga maji kwenye kinu, maana mateja wote sio wasikivu
ReplyDeleteKabisa mdau,kama anataka kujikomboa mbona kuna njia nyingi,na njia iliyo nyepesi ajipeleke mwenyewe kwenye kituo chochote aone kama hatapata msaada.
DeleteAANZE KWANZA YEYE MWENYEWE KUJUA TATIZO ALILONALO KABLA YA KUOMBA KUSAIDIWA!!!!MANAKE ANAONEKA HAKUBALI KAMA ANAKULA BWIMBWI. AWE MUWAZI ILI ASAIDIWE!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteAPOTEE ZAKE HUKO,KUNA WATU WANAHITAJI MISAADA NI BORA WASAIDIWE WAO KWANZA,KWA HUYU KAJITAKIA MWENYEWE AKAE KANDO KWANZA.
ReplyDeletekwani waliomfikisha hapo wako wapi?si aende makwao awombe
ReplyDeletewamsaidie.
EEEH!KUPANGA NI KUCHAGUA.
ReplyDeleteASAIDIWE NINI AU KWA LIPI?
ReplyDeleteMBONA YEYE MWENYEWE HAOMBI MSAADA.
..kuna dogo kafungwa maisha kisa kilo20 za mirungi sasa wewe umekamatwa na unga umeachiwa unataka usaidiwe nini? kama ushajua tatizo lako ni unga, maanake swala la kuacha ama la ni lako unataka nani akusaidie kuacha unga..amua acha endelea na maisha na ujifunze toka kwa makosa, mengine ni laana za uliowakosea,kwana wadhani hawana familia na hawasikii maumivu kutukanwa wakati hawakukukosea?
ReplyDelete