Lady Jaydee Ajibu Tetesi za Kurudiana na Gadner

Msanii mkongwe katika muziki wa bongo fleva, Lady Jaydee amefunguka kuhusiana na tetesi kwamba amerudiana na aliyekuwa mume wake Gadner G Habash.

Aliulizwa swali hilo na mtangazaji Sam Misago katika kipindi cha E News kinachorushwa na kituo cha EATV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa.

“Watu wengi walinipenda kama nilivyo na hawakunipenda nikiwa na mtu yoyote, sipendi kuelezea mambo yangu binafsi nawaomba watanzania wanipende kama mimi kama Jaydee na si vinginevyo,”alisema Jaydee.

Msanii huyo ameibuka tena na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Ndindindi ambapo amesema video yake ataitoa itakapokuwa tayari.

Chanzo:Bongo5

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hajajibu swali,swali lina jibu la 'ndio' au 'hapana'

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad