Maafisa wa Kenya, Akiwemo Katibu Mkuu wa Nishati Wadakwa Bandari ya Tanga

Maafisa kadhaa wa Kenya wakiwemo Katibu mkuu wa wizara ya nishati wameshikiliwa na maafisa wa uhamiaji mjini Tanga baada ya kujiingiza kwa siri katika msafara wa Waziri wa nishati wa Uganda aliyekuja nchini kufanya mazungumzo "ya siri" na serikali ya Tanzania kuhusu sakata la bomba la mafuta.

Wamenyang'anywa pasport na kuwekwa kizuizini mpaka mazungumzo yatakapoisha ndipo waruhusiwe kuuliza feedback ya kikao.

Jana Waziri wa nishati wa Uganda alikuja kufanya mazungumzo na serikali ya Tanzania kumbe jamaa walikua wamejichomeka kisiri na kujifanya nao ni Waganda, walipofika tu wakastukia wamefanyiwa umafia kwa kuzungukwa pande zote na kunyang'anywa passport zao.

Mashuhuda wanadai jamaa walibaki kulia lia tu wakaambiwa kaeni hapa mpaka tutakapo maliza mazungumzo ndipo mrudi kwenu, mpaka mida hii Waziri wa Uganda yupo kwenye mazungumzo na haijulikani hatma ya maafisa hao wa Kenya.

Naona Magufuli sasa anaanza kurudisha hadhi ya Tanzania, ule unyang'au nyang'au tuliokukwa tunafanyiwa na hawa wajinga sasa utakwisha.

UPDATE: Maafisa hao wameshaachiwa
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahahhahahahaahah daaah nimecheka jamn hahahahah aisee bomba limezua jambo chezea maendeleo wewe

    ReplyDelete
  2. It's about time, sleeping time is over

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad