Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Shariff Hamad ameondosha familia yake katika Kisiwa cha Unguja na kuipeleka Muscat-Oman.
Familia hiyo ya Maalim Seif Shariff Hamad wameondoka jioni hii kwa kutumia ndege ya Shirika la ndege la Oman (Omar Air). Familia hiyo ya Maalim Seif wameondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport saa 5:50 jioni hii.
Haikuweza kufahamika mara moja sababu hasa za Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Shariff Hamad kuiondoa familia yake Zanzibar. Kwa sasa Makamu huyo wa Kwanza wa Rais yupo katika mapumziko katika Hoteli ya Kitalii ya Dar es Salaam Serena.
Chanzo: ZanzibarNews.net
Haya tena sisi walalahoi tunaouwana kwa ajili ya mahaba ya vyama tukimbize wapi na sisi familia zetu au damu zetu ni halali kutolewa kafara kwa ajili ya CUF wajinga ndio waliwao
ReplyDeleteHapo chachaa ndio maana binadam tumepewa akili za kufikiri tunapotenda jambo. Baya au zuri. Linamanufaa kwako na jamii inayozunguka au halina.Maanake wapo watu wao wanajifikiria wao tu.sio wengine
DeleteYeye mwenyewe yuko Dar kwa mapumziko????????familia anaiondoa z'bar,???????Tunatakiwa tujiulize mara 100,nina shaka ya kwamba kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia.Tuwaombee ndugu zetu wa-zanzibar.
ReplyDeleteHiyo ndio kitu inaitwa SIASA...wanaokufa mara nyingi ni walala hoi na washabiki wa siasa,,, Nazichukia siasa!!!
ReplyDeleteHatujifunzi tu?
ReplyDeleteAsanteni.
ReplyDeleteSi yeye tu. Matajiri wote Unguja Pemba. Familia zao ziko Muscat. Dubai. UK. Dar.
Haya,sie hatuna pa kwenda ngoja tumuombe Mungu wetu,
ReplyDeletemaana Mungu wetu hashindwi jambo.
Mnayemtegemea yuko mapumziko tena kwenye hotel ya kifahari na familia inahamishiwa mbali na matatizo. Poleni sana walala hoi hata ela ya kitumbua hamna pia hamjui hatima ya maisha yenu. Amkeni Wazanzibar mmeachwa kwenye mataa....
ReplyDeleteMungu amlinde na kila lenye baya nayeye na tuko radhi tuu alivofanya kuondosha familia yake kwa sababu hiyo mijini yote inamtaka yeye na familia yake tatizo liko wapi kuondosha watu wake? haki itatendeka tuu inshaallah hamjijui muandikalo nyie nyote mulokua na ajabu nae.
ReplyDeleteM'mungu apishilie mbali. Awavize wote wenye nia mbaya na usalama wa wazalendo wa zenjibar. Damu nzito kuliko maji. Enyi maji amkeni wakati ni sasa mwenye macho haambiwi tazama. Enendeni mkachague sirikali ya wazalendo kwa amani na salama. Kila kheri inshaallah.
ReplyDelete