MAGUFULI tupatie mashamba tukalime baba, jana umeagiza tukamatwe, tupelekwe kambini tulime kwa lazima.
Hakuna haja ya kukamatwa baba, tupatie tu mashamba tutalima wenyewe, kule vijijini kila pori tunalogusa tunaambiwa la #MWEKEZAJI, kila shamba tunaloliona tunaambiwa la #MHESHIMIWAFULANI.
Hakuna mashamba ya wazi baba, hata serikali imegawa mashamba yake kwa #WADOSI.
Tusaidie pia na vitendea kazi, hata majembe ya #NGWAMBA tu baba. Mbolea Na umwagiliaji tutamwachia tu #MUNGU ataleta neema zake baba.
waangalie na TIB na Benki ya Kilimo baba kama mikopo yao inawafaa vijana unaowakurupusha leo!... Benki zako zinawafaa zaidi wazee kukopa kuliko sisi vijana baba.
Tafadhali sana baba usitufukuze tu bila kujua tutakapoelekea
By Habibu Mchange
MAGUFULI Tupatie Mashamba Tukalime Baba, Juzi Umeagiza Tukamatwe, Tupelekwe Kambini Tulime Kwa Lazima.
6
March 16, 2016
Tags
point taken bay presidaa
ReplyDeleteMTAFANIKIWA 100% KAMA KWELI MTAJIPANGA NA KUANDAMANA KWENDA KWA RAIS KUOMBA HAYO MNAYOTAKA,RAIS WETU ANAPENDA WATU WA KUJITUMA,ARDHI IKO YA KUTOSHA.MUNGU WETU AWATANGULIE.
ReplyDeleteWabongo kwa kunun'gunika na siasa za porojo mtawezekana wapi? Anachokizungumza Magufuli ni sahihi kabisa vijana wengi wa kitanzania hawajitambui huku wakiamini na kudream njia ya mkato katika kujipatia kipato kama njia muafaka. Hata kama hakuna ardhi ya kujiendeleza na kilimo ndio ukapoteze muda kwa kucheza bao asubuhi wakati unaweza ukaituma akili yako kufikri mambo ya maana zaidi na kuna mambo mengi tu ya msingi ya manufaa ya kufanya. Watanzania wengi ni watu wanaopenda vitu vya rahisi yaani sio watu wanaopenda challenge katika maisha. Believe me challenge au changamoto katika maisha ni sawa na changa ya kufanya mambo mema hapa duniani ili ukapate pepo. Na duniani vile vile bila ya kupata changamoto katika kuanzia maisha ni taabu kuja kurekebisha maisha yako yaje kuwa ya nafuu. Na kwa kukaa kwenye pool table kusubiri ardhi ikufikie hapo mtachelewa sana. Kwa sisi tuliobahatika kuishi huku nje nazungumzia hapa marekani kuanzia mtoto wa miaka kumi sita tayari keshafahamu hatma ya maisha yake ipo ndani ya uwezo wake. Mawazo ya kusema anategemea sijui serikali labda kaka au mama au baba sijui mjomba au rafiki ndio aje kumtengenezea maisha yake hilo halipo kabisa katika akili yake na ukimsaidia atakushangaa sana na pengine asiukubali msaada. Na itakuaje kijana mzima unanguvu na akili uishi kwa kusubiri msaada wa mtu hata kama wa mzee wako basi lazima ujiulize kwanini? Unaweza kukopa kama msaada pasipo na budi kwa maana yakwamba utaurejesha mkopo huo lakini usubiri mtu aje kukugaia kitu bure bure tu haiwezekani, si shangai wageni kuwa na ardhi wenyeji hawana kwa sababu sisi wenyewe ni wazembe na wapumbavu tunatakiwa kubadilika. Watanzania tuacheni upumbavu wa kumpigia vijembe vya kipuuzi Magufuli badala yake tunatakiwa kubadilika kwa manufaa yetu na nchi na vizazi vijavyo,time of change has come we need to wake up and participate on the movement.
ReplyDeleteMh Rais kwanza angeandaa mazingira ya ufanyaji kazi kwa vijana kabla ya kutoa amri ya kukamatwa kama hafanyi kazi na ikibidi apelekwe 'camp' kwa lazima akafanye kazi kule duuh!Watengenezee vijana wako mazingira ya huo utendaji kazi unaoutaka,waandalie ardhi,vitendea kazi,maji safi hata sehemu ya kulala ukiwawekea mahema kwa ajili ya kulala sio tatizo,wawekee security kwa ajili ya usalama wao,na vingine vya msingi ambavyo mwanaadamu anavihitaji,weka utaratibu wa masomo ya stadi za ufundi kwa vijana wasiotaka kilimo almradi asiwe yupo yupo tu mtaani,apate knowledge ya kiasi cha kuweza kumudu maisha pindi atakapomaliza mafunzo,vitakapokamilika hivyo baadhi nilivyovitaja,sasa mh Rais toa tamko la kijana asiyetaka kazi akamatwe na apelekwe kambini akafanye kazi kwa lazima,hivi hivi tu bila maandalizi,unaturudisha kipindi kileeeee cha Mw Nyerere,kipindi cha nguvu kazi,kwenda Gezaulole na Kivugumo pasimo maandalizi ya kutosha nakumfanya mtz aishi kwenye nchi yake kwa mateso,,,,,,na hii ni tanzania ya Digital sio ile ya Mwalim,dunia sasa imekuwa kama kijiji taarifa zinasambaa ndani ya dk tu dunia nzima,so be care na maamuzi ya kukurupuka,tunakuunga mkono lkn kwenye kukurupuka tutakupa kuntu Magufuli.
ReplyDeletekamata tuu
ReplyDeleteinaboa sana kukuta kijana anacheza pool asubuh afu waze wako mashamban
Halafu mtu anadai waandaliwe mazingira,mazingira gani sasa?mbona wengine baada ya kumaliza vyuo na kuona ajira ngumu tumejiajiri?hivi mikopo yote hiyo mtu unashindwa kukopa hata kufungua genge au kuosha viatu,magari nk badala yake uende kwenye pool?INABOA.
Delete