Malawi Yatekeza Tani Mbili za Pembe za Ndovu Kutoka Tanzania Zilizonaswa na Maafisa wa Usalama wa Nchi Hiyo..

Malawi imeteketeza tani 2.6 ya pembe za ndovu ambazo zilinaswa na maafisa wa usalama zikitokea nchi jirani ya Tanzania.

Meno hiyo 781 ya tembo ambayo inakisiwa kugharimu takriban dola milioni tatu ilipatikana baada ya operesheni dhidi ya ulanguzi na uwidaji haramu.

Mkurugenzi wa idara inayosimamia mbuga za wanyama pori Bright Kumchedwa, amesema kuwa hiyo ni ishara ya kwanza na dhabiti kutoka kwa Malawi kuwa haitaruhusu tena ardhi yake kutumika kulangua bidhaa za uwindaji haramu.

Hafla ya hiyo ya kihistoria ilifanyika katika eneo la Mzuzu kaskazini mwa nchi hiyo.
Kenya inatarajiwa kutekeleza hatua kama hiyo mwishoni mwa mwezi huu, Kenya imekamata takriban tani 120 ya meno ya ndovu.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Da hii nchi. Ya Tanzania ina matatizo makubwa. Tena ni aibu kwa taifa. Wanyama wanaowaletea pato la utalii wanazidi kuwamaliza kwa kuwangamiza. Kwa utajili wa muda mfupi. Hawa wanyama wakipotea ni generation kwa generation hawatakuwepo tena. Hii nchi haina maadili wala hawapendi fuata sheria.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad