Marekani Yasitisha Msaada wa Mabilioni ya Pesa Kwa Tanzania...Watoa Sababu Hizi Hapa

Shirika la ufadhili la serikali ya Marekani limesitisha msaada wake kwa serikali ya Tanzania likilalamikia matukio kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kutekelezwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao.

Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imesema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja za Tanzania.

Kupitia taarifa, bodi hiyo imesema: "Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.”

Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao "haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa.”

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ali Mohammed Shein alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani, Chama cha Wananchi (CUF).

MCC imesema kwamba huwa inatilia mkazo sana demokrasia na kujitolea kwa nchi kufanikisha uchaguzi huru na wa haki.

"Uchaguzi uliofanyika Zanzibar na kutekelezwa nwa Sheria ya Uhalifu wa Mitandao vinaenda kinyume na hili,” imesema.

Tanzania ilipokea Dola 698 milioni katika awamu ya kwanza.

Pesa za MCC hutumiwa kufadhili miradi ya maji, barabara na nishati.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Big Liars,,,son of the bi,,,,ch

    ReplyDelete
  2. Safi sanaaaaa hahahahhahah nimefurahi

    ReplyDelete
  3. msilete misaada mkileta wanagawana mafisadi hamna maji na barabara za mikoani zimejaa mashimomashimo, lami zimebanduka ovyo.. hii nchi no demokrasi kuna wakuru wanabaka demokrasi.

    ReplyDelete
  4. Wachina watakuja

    ReplyDelete
  5. kweli hiyo misaada wanalamba wenyewe mafisadi sisi haitusaidii kitu,kwa hiyo wamarekani nyie kaeni na hela zenu hawa watu huku ni wezi watupu.

    ReplyDelete
  6. Tatizo sio misaada. wanaleta tujimisaada alafu wanahiba mihela katika bara hili, mpka baadhi ya viongozi wao huko ulaya walisha kili. kwa kwamba tunatoa misaada kidogo sana Africa, lakini Africa inatoa mihela kibao, ndio maana nasi tunazidi endelea na watu wetu kuishi vizuri na Africa inaendlea kuwa masikini,na watu wao kuishi hovyo hovyo vibaya kwa kuwa wafrica hawajielewi, kwa kila nyanja. kuanzia uongozi, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni, ni bara jeusi, balo alijamka, ukichukulia na viongozi wengi wanadai ni kina sultani mangungo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad