Mgombea wa Urais Marekani Donald Trump Ashutumiwa Kuwa ni Tapeli...Atakiwa Kukatwa


Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Mitt Romney amekitaka chama chake kumkataa Donald Trump ,akimtaja mgombea huyo aliye kifua mbele kuwa ”tapeli”.

Bwana Romney amemshtumu Bwana Trump kwa kuwachukulia raia wa Marekani kama wajinga katika hotuba ya siri iliotolewa kwa vyombo vya habari.

Bwana Trump hatahivyo amemkejeli bwana Romney katika mtandao wa tweeter kama mgombea aliyefeli na ambaye hafai kutoa ushari wowote kuhusu uchaguzi.
Viongozi wakuu wa chama cha Reupblican wameshangazwa na vile bwana Trump anavyoelekea kushinda tiketi ya chama cha Republican kwa uchaguzi huo wa mwezi Novemba.

Inadaiwa kuwa wanachama kadhaa wa kamati ya kitaifa kuhsu usalama wa jamii waliandika barua ya wazi wakielezea maono ya bwana Trump kama yasio na msingi wala sera.

Bwana Trump amejiwasilisha kama muunganishi kufuatia ushindi wake katika majimbo saba katika ile ilipotajwa kuwa jumanne maalum na hivyobasi kuimarisha uongozi wake katika chama chake.

Romney ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Trump anatarajiwa kutoa onyo katika hotuba yake siku ya Alhamisi,kwamba sera za bwana Trump ni tishio kwa chama cha Republican na taifa zaima kwa jumla.

Bwana Romney pia ataonya kuwa uteuzi wa Trump utarahisisha harakati za Bi Hillary Clinton kushinda urais nchini humo.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hategemei pesa za chama ana fweza km njugu hafilisi mtu anasema atakacho nakufanya apendavyo sio kutegemea pambe za uswailini na Dabe nyingi

    ReplyDelete
  2. yARAABI HEBU ONYESHA MIUJIZA YAKO BW, TRUMP ACHAGULIWE KUIONGOZA MAREKANI KISHA DHAMIRA YAKE ITIMIE KUWAKAMATA MARAISI WOOTE WA AFRIKA ( MATAPELI)

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad