Ni ukweli uliodhahiri kwamba kwa sasa mjadala ulioteka kila kona ya nchi ni jina la Katibu mkuu mpya CHADEMA.
Kwa mujibu wa Katiba ya chama Mwenyekiti ndiye mwenye mamlaka ya kupendekeza jina la Katibu mkuu na hatimaye kupigiwa kura na Baraza Kuu.
Jumamosi ya wiki hii nchi inatarajiwa kutikisika kwa tukio linalosubiriwa na mamilioni ya wafuasi wa Chadema kote nchini ambapo kutokea jijini Mwanza moshi mweupe utaonekana pale Freeman Mbowe atakapoibua jina la Katibu Mkuu.
Shauku ni kubwa kutokana na ukweli kwamba Chadema ndicho chama kikuu cha upinzani nchini kikiwa na mashabiki kila kona ya nchi.
Pia sababu nyingine ni kutokana na mazingira aliyoacha Katibu mkuu wa zamani Wilbroad Slaa ya kususia uongozi baada ya kukosa fursa ya kugombea Urais.Ususiaji ambao unadaiwa ulisababishwa na mkewe Josephine Mushumbusi.
Pia chama hicho kinajaza nafasi hiyo huku kikiwa na hazina kubwa ya wanachama maarufu wakiwemo mawaziri wakuu wawili wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye.
Yote kwa yote Freeman Mbowe ndiye anatarajiwa kutegua kitendawili hiki huku wafuasi wake wakimpa jina la utani..' mzee wa kubadili gear angani..''
Tusuburi tuone...
Charity starts at home! Nilini vyama vya upinzani vitaanza kuonyesha demokrasia kwa vitendo kwa watu kama akina Mbowe, Maalim Seif nk kung'atuka na kuchia fresh blood?
ReplyDelete