Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), David Mattaka, amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuliingizia serikali hasara ya Dola za Marekani 772,402.08.
Akisoma mashtaka hayo jana, Vitalis Thimos, wakili wa serikali mbele ya Respicius Mwijage, Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu alisema kuwa, mshtakiwa huyo anakabiliwa na kosa hilo kutokana na matumizi mabaya ya madaraka katika ofisi ya umma.
Tuhuma hizo ni pamoja na kutia saini mkataba wa kukodisha ndege aina ya Air bus A320-214 kwa Kampuni ya Wallis TradingInc bila kufuata sheria na taratibu za zabuni.
Mattaka anadaiwa kuiingizia hasara serikali kutokana na hatua yake ya kuidhinisha pesa za matengenezo ya ndege hiyo katika Kampuni ya AEROMANTENIMIENTO.
Hasara nyengine ni matumizi mabaya kwa kununua vifaa vya ndani ya ndege hiyo yaliyoigharimu Dola za Marekani 35,984.82.
Watuhumiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Ramadhani Mlinga, Mkurugenzi wa Manunuzi ATCL na Bertha Soka ambaye ni mwanasheria wa shirika. Watendaji hao wanadaiwa kushindwa kuzuia ubadhilfu huo. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 19 Machi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), David Mattaka Ashitakiwa Tena Kwa Uhujumu Uchumi
1
March 16, 2016
Tags
KILA MAHALA NI HUOZO
ReplyDelete