Msomi Prof Baregu Aibuka na Kudai Utawala wa RAIS Magufuli ni wa Kejeshi...Kuwapo Kwa Wanajeshi Wengi Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa Wamtisha

SIKU moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kuteua wakuu wa mikoa wapya, mtaalamu wa sayansi ya siasa, Profesa Mwesiga Baregu, ameibuka na kusema kuwa kuwapo kwa wanajeshi wengi wastaafu katika uteuzi huo inadhihirisha wazi kuna dalili za utawala wa kijeshi nchini.

Profesa Baregu amesema kuwa  wanajeshi huwa hawana hulka ya kidemokrasia.

“Kitu kimoja kinachojitokeza kwenye uteuzi huu ni kuwepo kwa wanajeshi wastaafu, na mimi ninavyoelewa wanajeshi huwa hawana hulka za kidemokrasia. Hii inaonyesha wazi kwamba utawala huu ni wa kijeshi,” alisema.

Profesa Baregu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema haileti picha nzuri kuwapo kwa wanajeshi wengi katika utawala kwa sababu tawala za mikoa na wilaya ni saula la kiraia na demokrasia zaidi.

Alisema rasimu ya katiba ambayo yeye alikuwa mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ilipendekeza kupitia upya tawala za mikoa na kupunguza idadi yake.

“Kutokana na hilo, mamlaka ya wananchi inamezwa kwa sababu wakuu wa mikoa na wilaya ni wengi na kunakuwepo na mgongano mkubwa,” alisema.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ali, alisema uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya ni wa rais na wanaoteuliwa ni watu mchanganyiko.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (Ruco), Profesa Gaudence Mpangala, alisema kila anapoingia kiongozi mpya anaunda timu ambayo anaona ataendana nayo.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuwepo kwa Wanajeshi, kwa upande wangu ni MZURI sana kwa sababu wa Tanzania tumezoea serikari za wizi za kiraia, kwa hiyo tunahitaji BAKORA ili tuondokane na karaha za ufisadi na rushwa zinazotawala nchi yetu yenye utajiri mwingi unaoliwa na wachache. Kwa hiyo sioni ubaya wa KUWEPO KWA WANAJESHI SERIKALINI.....HAPA KAZI TU NA BAKORA KWA WINGI

    ReplyDelete
  2. hapa kazi tu. Tumechoka kuvumiliana na kubebana.

    ReplyDelete
  3. Kaza kamba JPM.Wakijituma ujangili wote utaisha. Pia ni hatari kwa wanajeshi kutokuwa na kazi so big up JPM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad