Mwanafunzi wa Kidato cha Pili Ampachika Mwalimu Mimba....

WAKATI ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za kielimu kutokana na kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako mwanafunzi wa Kidato cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu wake.

Mwanafunzi huyo aliyemzalisha mwalimu wake ana umri wa miaka 17, wakati mwalimu huyo anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya Umma ya Nkasi, iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka 25.

Tukio hilo linalotajwa kuwa la kwanza kutokea wilayani hapa, limekuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa Nkasi na wilaya jirani.Hata hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa wakimpongeza mwenzao kwa kujaliwa kupata mtoto katika umri wake huo mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na uhakika wa maisha kutokana na kuwa ni mtumishi serikalini.

Imeelezwa kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi wake bado anaendelea na masomo shuleni hapo, huku `mzazi’ huyo wa kiume akifundishwa na mzazi mwenzake.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Namanyere hivi karibuni.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkasi mjini Namanyere ambayo ni ya mchanganyiko ya umma, Amiamie Nanga alisema mwalimu huyo alianza kazi shuleni hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufundisha baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu chuoni.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sheria inasemaje maana mwanafunzi yuko chini ya miaka 18 je, amebakwa?

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  3. Huyo mwalimu achukuliwe hatua za kisheria, hairuhusiwi mwalimu na mwanafunzi kuwa na uhusiano wa kimapenzi, hivyo sheria uchukue mkondo wake, kama ilivyo kwa walimu wa kiume.

    ReplyDelete
  4. Mambo hayo ya kupenda ndogondogo kwa ajili ya pumzi myfuuu

    ReplyDelete
  5. Elimu ya kujamiiana lazima ifanywe practical.mwalimu amemfundisha kijana .kosa liko wapi?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad