Mwanamuziki Diamond na Mtoto wake Tiffah Wapima DNA Sauzi

Hii ni EXCLUSIVE stori! Kufuatia kelele kibao kutoka kwa wadau mbalimbali kwamba mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, yaani Latifah ‘Tiffah’ aliyemzaa na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ si wa nyota huyo, hatimaye, jamaa ameamua kupima vinasaba ‘DNA’ (DeoxyriboNucleic Acid).

ISHU ILIKUWA AFRIKA KUSINI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Diamond aliamua kutekeleza mpango huo nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambako aliamini hakuna ‘macho mengi’ ya watu, hususan mapaparazi.

SIKIA HII
“Jamani mimi nataka niwape stori ambayo ni ya uhakika. Hivi mnajua kwamba Diamond aliamua kwenda Sauzi kupima DNA yake na mtoto wake Tiffah?
“Kutokana na manenomaneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda. Hivyo ili kuondoa figisufigisu, akamwambia Zari waende wakampime DNA mtoto na yeye. Ni kabla hajaenda Marekani.”

MAJIBU HAYA HAPA
Chanzo hicho kikasema: “Majibu ya DNA yamesema, Nasibu Abdul ni biological father (baba wa damu) wa mtoto Tiffah. Ilibidi jamaa amwage chozi maana alifikiria mengi, watu wamesema sana kuhusu yeye na Tiffah, kwamba si mwanaye, mara ni mtoto wa Ivan (Ssemwanga, mtalaka wa Zari), mara ni mtoto wa pedeshee mmoja wa Bongo. Yaani mengimengi yalisemwa.”

Chanzo: GPL

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. haya ampime na bongo tuone kama rafiki yake Ney.

    ReplyDelete
  2. kila kitu wamefanya siri majibu hatujayaona bibi masumboko na domo waongo.

    ReplyDelete
  3. FIX NYINGINE HAZINA TIJA. FAKE DNA FAKE MAHUSIANO.

    ReplyDelete
  4. Hakuna kitu kama hicho ni uongo mtupuuuu wasitudanganyeee,lol...diamond mara tumepima ocean road! Mara South Africa ni uongo mtupuuuu mbona aliambiwa afanye OPEN DNA akakataa????aache uongo 90 percent ya watanzania wote tunajua mtoto sio wake na yeye anajua piaa!!!!!anataka tuu azungumziwe kwenye magazine basiii....tumeshakuchoka kwa uongo tafuta jipyaaa

    ReplyDelete
  5. Kwanini south??? Hata wakienda USA who caresssss,,,math,,,fu,,,,k

    ReplyDelete
  6. sasa nyie apo juu mnachoumia nin?
    mbona watu mnarohoo za hasidi kiasi icho
    yani mtu kasikia tiffa ni mtoto halali wa domo eti ana panick
    wabongo bhana ni shida

    ReplyDelete
  7. mmekomaa na DNA ya Tiffa manina zenu......mlimzaa nyie????Kapimeni zenu na baba zenu ili mjue maana hao mnaowaita baba baba huenda sio baba zenu mbuzi nyie. Waacheni Mondi na zari walee mtoto wao kwao wao ndo wenye mtoto na wanaojua hilo

    ReplyDelete
  8. wivu wenu tu na nyie kapimeni na baba zenu muone kama ni kweli baba zenu!!!

    ReplyDelete
  9. Hivi mnadhani Zari ni mjinga kiasi gani kumbambikia Dai mtoto wakati anajua hizi ni zama za uwazi?
    Hata huyo Daimond kaamua tu kwenda kupima kwa ile hali ya kusema lisemwalo lipo ili ajiridhishe.wanaotoa mapovu ni wale wanamuona Tiffah kwa picha tu.Tee kafanana na Dai,kuna vitu vingi sana anafanana nae,mnaochonga jitahidini mkamuone sio kuhukumu kwa picha tu.

    ReplyDelete
  10. Hahahaha! Cinema?? Ndio kusema hii movie imekwisha au bado itaendelea??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad