Mwanamuziki Malaika Amefunguka Kuhusu Tetesi za Kuhongwa Gari Aina ya Ranger Rover...

STAA wa Ngoma ya Zogo, Diana Exavery ‘Malaika’ kwa mara ya kwanza amefungukia gari jipya la kifahari analodaiwa kumiliki aina ya Range Rover Sport kuwa hajahongwa kama watu wasemavyo.

Akichonga na Showbiz, Malaika aliyewahi kubamba pia na Ngoma ya Sare Sare na Mwamtumu alisema kuwa katika picha ambayo aliachia kwenye ukurasa wake wa Instagram hivi karibuni ni kweli gari lake na kwamba hajahongwa na mtu.


“Ni kweli lile gari ni la kwangu na nipo katika utaratibu wa kulishughulikia litoke bandarini, sijahongwa na mtu jamani hao wanasema tu ila mimi nimesema nilichosema inatosha,” alisema Malaika.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa nyimbo zipi na shoo ipi ununue range rover nyie mabinti jamni hebu acheni kutudanganya na kudanganya watoto wetu waone kwamba unaweza kuimba wimbo mmoja bila shoo na ukanunua range manwafanya wasitake shule waamini sanaa yenu inalipa balaa diamond huyo hapo ame hustle mpka kumiliki prado ni baada ya shoo kadhaa na nyimbo kibao iwe wewe nyimbo 2 siziso na shoo ununue range jamn eti sijahongwa sawa inawezekana umepewa zawadi basi si useme.ukweli.ukipokonywa ooh unajua ilikuwa hv ikawa vile pumbavuuuuuu...kumbe na ww ni wale wale....mala@@!#@&#^y fulani amazing. .mfyuuuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. usiumie na wivu,. kwani amekwambia anategemea music tu?

      Delete
  2. Kwani hata ukihongwa kinawauma nini uchumi si wako akuwacheee kutesa kwa zamu

    ReplyDelete
  3. Mie nasema..Mradi unaweza kulipa TRA. Na liko kihalali na pesa za mawese zipo.. Dada ponda maisha.. Ila angalia Wema na Aunty.. TRA wako nyuma yao..sasa na ww yasije kuwa ndiyo hayo hayo...JP TUKO FIT

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad