Tanzania tutegemee kuingia kwenye shida ya kiuchumi. Wale washirika wetu wa maendeleo yaan zile nchi za ulaya. Kwa kauli ya pamoja wamesitisha misaada katika nchi yetu.
Tukumbuke misaada yao inaingia moja kwa moja kwenye bajet!! Wanaojua hatujitoshelezi. Kimaneno tunajitosheleza kwa 60% kivitendo hatuzid 40%.Ni zaid ya ile MCC. Maamuzi hayo yamekubaliwa na nchi 10 kati ya 14 za Umoja wa ulaya.
Swali kwa watawala hata hizo milijua hamtapewa mlijiandaa kujitegemea??
Maana ya MCC nilimsikia msemaji wa wizara ya fedha anasema waljua haztakuja hawakuziweka kwenye bajet.
Je na za washirika wa maendeleo hamkuziweka???
Wananchi mnatwambia tufunge mikanda suruali zetu zinavyotupwaya wakati nyie mnashindwa Hata kufunga vifungo vya makotI kwa vitambi.
Chanzo:Jamii Forums
Chanzo:Jamii Forums
Haaahahha tufunge mkanda wakati suruali zinatupwaya hahahhaha uwiii wao wanashindwa kufunga makoti kwa mavitambi yao hahhahaa daaah hii sentensi imeniua mbavu...
ReplyDeleteWatanzania wote tukiwa kitu kimoja kwa kauli ha hapa kazi tu,na kwa kumaanisha kamwe hatutafunga mikanda,Tuache ufisadi,tulipe kodi ipasavyo,tuache magendo,tuache kupeana mishahara hewa nk.
ReplyDeleteUkikuta mtu kama wewe unashangilia nchi yako kunyimwa misaada ina maana upo tayari kuuza utu wako kwa watu wengine.wamarekani ni wanafiki cyber crimes kwao ni serious issue ikija kwetu ni tatizo wakati wao wanachunguza simu zote na unaweza kukamatwa without notice but kwetu ni tatizo wakubali tu tumechagua mtu asiyetaka mikataba mibovu kama ya kwao ndio maana wanaona maslai yao yameguswa mtu waliyetarajia kuchukua nchi tumempiga chini.tutakomaa tu.
ReplyDeleteKwani kipi cha ajabu?mbona wazee wetu walifunga mikanda enzi za vita vya uganda ya Idi Amin na tanzania na bado walivuka?Kwani hao wenye kushindwa kufunga makoti kwa vitambi hawakuwepo?
ReplyDeletehiyo ndo ccm kila kukicha inazidi kutumiza tutakua kama zimbabwe
ReplyDeleteCCM ITABAKI KUWA CCM,WA-TZ HAPA TUKO KI-MAGUFULI,KI HAPA KAZI TU ILI TUSONGESHE NCHI YETU KWA MANUFAA YA KILA M-TZ.
DeleteHakuna cha ubabaishaji tumechoka kupangiwa utaratibu this time watatujua sie ni nan na lazma ukoloni mamboleo ufike kikomo hakuna ncgi kiranja ndani ya nchi za watu wengine.nchi ngapi hazipati misaada?toka JPM aendelee kuharibu madili yao nao wanakazana kutaka kuleta timbwili tuko macho pima.fyuu na ukibaraka wenu mnawaheshimu weupe?laana
Deletekwani umeambiwa magufuli ni yesu......ni mwana ccm huyo utakua mwehu kama unamfurahia magufuli halafu hutaki kusikia kuna ccm.......
ReplyDeleteMi nimefurahi sana, kwani hiyo misaada yao sisi tumewaomba? Tena hii itatusaidia sana kujifunza kujitegemea. Hata hivo misaada yao wala haitusaidii lolote zaidi ya nchi zao kufaidika nayo. Unaona kama biashara ya wakimbizi ilivo, ni hao hao wagunzu wanaosababisha vita ktk nchi zetu ili wafanye biashara ya kutuibia waafrika maliasili zetu mfano DRC Congo, soko la kuuza bidhaa zao kama magari, mafuta na kuja kujilipa mishahara ya kufuru kwa kujipatia vyeo vya juu kwenye hiyo wanayoita miradi ya maendeleo.
ReplyDeletehapa kazi tu ni kuokota chupa za maji zilizotupwa na kuimarisha biashara ya vyuma chakavu, kila mtu afanye kazi yake kwa bidii HAPA KIZA TU!
ReplyDeleteKinachotupata sasa hivi ni matokeo ya uongozi mbovu wa awamu ya nne, ulio kumbatia wezi na wahujumu uchumi.
ReplyDelete