Ni Kipi Hasa Kilichomuondoa Balozi Ombeni Sefue Ikulu? Atapangiwa Kazi Gani Nyingine?

Tumekuwa tukipaza sauti kuwa mtu anayeondolewa kwenye nafasi yake ya utumishi basi ni lazima zitolewe sababu za msingi za kuondolewa kwake! Haiwezekani katibu mkuu kiongozi anaondolewa kimyakimya tu huku tukiwa hatupewi sababu za kuondolewa kwake!

Kiongozi huyu alikuwa akitoa matamko mbalimbali huku rais Magufuli mwenyewe akituaminisha kuwa ni mtu wa viwango na anayekidhi kile anachokiita "speed yake" Leo kulikoni?

Hatupingi kuondolewa kwa watu hawa kama wamefanya makosa! Lah! Tunapinga namna wanavyoondolewa huku kukiwa na sintofahamu ya hali ya juu!

Tulishuhudia Daktari Hoseah akitenguliwa uteuzi wake kimyakimya! Pia wapo watumishi wengine wengi huku mambo lukuki yakifichwa!

Sasa leo tunaambiwa kuwa Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine? Ipi? Cheo cha katibu mkuu kiongozi ni cheo cha nne kwenye mhimili wa serikali! Atapangiwa kazi gani? Waziri mkuu? Makamu wa rais? Rais? Kutumbuliwa kwake kunaonyesha kuwa alikuwa na kasoro katika utendaji wake na si vinginevyo! Zipi?

Hali hii ya kufukuzana kimyakimya inaweza kuzua uhasama wa aina yake nchini! Kwanini mtu akifukuzwa na au kusimamishwa kazi zisitolewe sababu za msingi zilizopelekea kuondolewa? Nini tatizo? Tunajenga nini?

Angalizo kwa wana JF: Wakati Ombeni Sefue akitoa matangazo mbalimbali wengi wenu mlikuwa mkishangilia! Wengine mkadiriki kuandika kuwa Ombeni, Magufuli na Majaliwa wanatosha kuendesha nchi! Mkasema kuwa hakuna haja ya baraza la mawaziri! Leo Ombeni Sefue anatenguliwa mnashangilia kwa maandiko mbalimbali! Mmesimamia wapi? Hamuoni kasoro za wazi kwenye huu utenguaji wa watumishi (baadhi yao? ) Mimi ni miongoni mwa wale tunaoamini kuwa, kama ni kusafisha kwa kwelikweli! Hata Magufuli mwenyewe ni jipu!
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mwachie Mh ayatumbue, siyo lazima ujue sababu, hayo majipu yanajulikana tu!

    ReplyDelete
  2. Sasa wewe unalaumu ama unatoa maoni yako? tatizo tulishazoea hali ya mazoea kuleana leana tu, hata kama mtu alikuwa anafanya kazi nzuri haimzuiii Raisi kumuondoa endapo amegundua kasoro, na labda kwa kumheshimu Sefue, siyo lazima zitolewe sababu kwa jamii, ukijua hizo sababu zitakusaidia nini kwa mfano? ama ni ili sasa tupate vya kuongea zaidi?
    Wapo waovu wengi na kwa kasi ya JPM watu wamevaa ngozi ya kondoo kwa sasa, na huwezi kumhukumu mtu kwa kauli za kusikia bila evidence, pale mtu akithibitika ana mapungufu na kwa staili ya JPM ni termination basi wafukuzwe tu, ni lazima nidhamu irudi na watu wafanye kazi kwa maslahi ya taifa tuache upuuzi wa kulaumu laumu ujinga tu

    ReplyDelete
  3. Watu bwana!
    Tumeambiwa Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine,sasa hapo ni swala la kusubiri,tukiona kimya ndio tuhoji.

    ReplyDelete
    Replies
    1. nafasi aliyekuwa nayo kama katibu mkuu kiongozi hakuna kazi nyingine yakupangiwa labda apewe uwaziri mkuu, makamu wa raisi au rais wa Zanzibar!! huyo kesha tumbuliwa! na ametumbuliwa kiheshema tu!

      Delete
  4. Jamani mbona kama mnashangaaaa??????.........mnakuwa kama mmeusahau ule uteuzi wa NSSF uliodumu kwa masaa matano??????........Angalieni jamani hicho kitu kilikuwa kinamhusu huyo mtu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad