Kufanyiwa upasuaji mara 13 si kitu cha mzaha. Na tena kwa tatizo lenye maumivu makali kama la Endometriosis. Kipi kinachompa nguvu ya kuendelea kuinuka na kupaza sauti kuhusu tatizo hilo?
“Ninaamini kila mtu ana matatizo,” anasema Millen.
“Ukiyachukulia matatizo yako kuwa ni makubwa kuliko mwingine hilo linaweza kuwa tatizo kwasababu utakaa ndani utadhani kuwa ni wewe peke yako mwenye tatizo hilo. Kwangu mimi nimekaa na hili suala kwa miaka 23 mpaka naamua kuongea hili suala mwaka jana. Mimi kwanza nina familia yangu, wadogo zangu wananiangalia lakini kwa sasa nina zaidi ya familia, wasichana wadogo wananiangalia,” ameongeza.
“Ninajitahidi kuwaonesha kwamba chochote unachoumwa, tambua kuwa haupo peke yako. Na mimi kuwa nje kujaribu kuwa hai inanifanya nijisikie vizuri sababu inanifanya niwe hai tena. Nikiwa hivyo watu wanaoniangalia nao wanakuwa hivyo pia.”
Kwa sasa Millen anawaomba Watanzania kuendelea kumuunga mkono kwenye kampeni yake ya #13IsEnoughFindCure4Endo.
huo ugonjwa uliukua nao si rahisi kupata support au msaada kwa watanzania sababu kwanza kwanza ulishawahi kusema kuwa wewe ni mgumba kutokana na ugonjwa huo kwa Tanzania mtu ukiwa mgumba yaani ni kama mtu hauna thamani tena yaani usipopata mtoto watu hawatokuheshimu wewe ni mtanzania lazima hayo unayaelewa, na wanaume wabongo huwa wakioa wanataka mtoto usipoweza kuzaa anakuacha anaenda kuoa mwanamke mwingine. kwa hiyo yaani kwa watanzania hata ukienda kwenye magazeti na mitandao yote unaomba support watu watakaa kimya tu, kama ni kusupport wangekuwa wameshakuunga mkono tangu zamani sababu ni mda tangu utoke wazi na ugonjwa huo, na ugonjwa huo upo kweli, si watanzania tu bali pia ulaya wanawake wenye ugonjwa huo wanapata tabu sana kutokana madaktari wanafikiri wanawake wanadanganya kuhusu ugonjwa huo, sisi wanawake hatuna thamani tunaonewa,mpaka wanaume ambao wanakula unga wanapata msaada lakini kwa wanawake ambao wenye ugonjwa ambao hauna tiba hawapati support au msaada
ReplyDelete